Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hawa ndio mastaa wa Uingereza ghali zaidi duniani

Mastaa Pc Ghali Hawa ndio mastaa wa Uingereza ghali zaidi duniani

Fri, 30 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo wa West Ham Declan Rice anauzwa bei ghali sana huku Manchester City na Arsenal, wakigombea saini yake kwenye usajili huu majira ya kiangazi.

West Ham inataka Pauni 100 milioni ndio ikubali kumuachia kiungo wao mahiri ambaye alikuwa na mchango mkubwa akiisaidia timu yake kubeba ubingwa wa Conference League msimu uliopita.

Sasa kiungo huyo huenda akaondoka kwenye dirisha hili la usajili lakini sio bei chee kwahiyo timu zijipange haswa kama inahitaji saini yake.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 aligoma kusaini mkataba mpya, akifosi West Ham imuuze huku taarifa zikiripoti ameonyesha nia ya kujiunga na Arsenal.

Miaka ya hivi karibuni wachezaji kutoka Uingereza wamekuwa wachezaji ghali zaidi duniani na kama unataka kuwasajili basi ujipange, mfano mzuri Jack Grealish alinunuliwa kwa Pauni 100 milioni na Man City kwenye dirisha la usajili la kiangazi mwaka 2021.

Gazeti la Dail Mirror limeorodhesha mastaa wengine kutoka Uingereza waliosajiliwa kwa pesa ndefu kwenye madirisha tofauti ya usajili.

Jude Bellingham - (Real Madrid, Pauni 88.5 milioni)

Uhamisho huu bado hauwezi kupondwa kwasababu kiungo huyo mwenye umri wa miaka 19 yupo kwenye orodha ya wachezaji wa Uingereza walionunuliwa kwa pesa ndefu.

Real Madrid ilijipinda na ikafanikiwa kunasa saini yake kutoka Borussia Dortmund kwa Pauni 88.5 milioni. Mashabiki wa Madrid wanatarajia mambo makubwa kutoka kwake baada ya kukiwasha Bundesliga.

Harry Maguire - Man United, Pauni 78 milioni

Maguire alikuwa beki ghali aliposajiliwa na Manchester United kwa Pauni 78 milioni. Hata hivyo kwasasa beki huyo anapondwa na mashabiki kutokana kiwango chake kibovu alichoonyesha miaka ya hivi karibuni.

Mashabiki wengi wa Man United wanashikiza beki huyo auzwe kipindi hiki cha usajili wa kiangazi. Licha ya kuwa nahodha wa timu beki huyo alisugua benchi msimu uliopita chini ya kocha Erik ten Hag.

Jadon Sancho - Man United, Pauni 72.9 milioni

Sancho alikuwa hatari alipokuwa akikipiga Borussia Dortmund, lakini licha ya kusajiliwa kwa mkwanja mrefu miaka miwili iliopita lakini kiwango chake bado hakijardhisha. hata hivyo kocha Erik ten Hag anaamini winga huyo ana kipaji cha kucheza soka, anachopitia ni jambo la kawaida kwa mchezaji. Msimu uliopita Sancho alipelekwa Uholanzi akafanye mazoezi ya peke yake ya kujiweka fiti.

Ben White - Arsenal, Pauni 50 milioni

White alikuwa akicheza beki wa kati kabla ya kuhamishwa kucheza pembeni, kiwango chake kikaendelea kuimarika Arsenal ikamnunua kutoka Brighton kwa Pauni 50 milioni.

Beki huyo wa kimataifa wa England amejumuishwa kikosi na Mikel Arteta mara kwa mara msimu uliopita. Kiwango chake bora kimshawishi Arteta na kumuamini.

Raheem Sterling - Man City, Pauni 49 milioni

Manchester City ilivunja beki ilipomsajili Sterling kipindi hicho alikuwa akikipiga Liverpool. Sterling alijiunga na Man City mwaka 2015 lakini kiwango chake kikawa bora zaidi kuanzia mwaka 2017.

Alifunga mabao 20 misimu mitatu mfululizo. Hata hivyo baadaye akapoteza namba ya kudumu na akauzwa na Pep Guardiola. Kwasasa anakipiga Chelsea.

Aaron Wan Bissaka - Man United, Pauni 49 milioni

Ole Gunar Solskjaer alimsajili Wan Bissaka kipindi anainoa Man United. Huu ulikuwa usajili wa kwanza wa kocha huyo kabla ya kufukuzwa kazi.

Aidha kwasasa hatima yake bado haieleweki na huenda akauzwa kwenye dirisha hili la usajili la kiangazi.

Kyle Walker - Man City, Pauni 45 milioni

Walker ndio alikuwa mchezaji wa kwanza kuondoka Tottenham akasake maisha mapaya sehemu nyingine. Kutokana na ubora wake Man City ikawekwa ofa mezani na ikasamjili kwa Pauni 45 milioni.

Walker amepata mafanikio mengi tangu alipotua Etihad. Msimu uliopita aliisaidia timu yake na ikabeba mataji matatu (FA, Ligi Kuu, UEFA).

Chanzo: Mwanaspoti