Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hawa ndio mabeki bora wa kulia

97030 Beki+pic Hawa ndio mabeki bora wa kulia

Wed, 26 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Wakati Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa imefika mzunguko wa 23, Simba, Azam na Yanga zinapewa nafasi ya kutwaa ubingwa msimu huu.

Pia timu 10 zinazoshika kuanzia nafasi ya 10 hadi 20 zimejiweka katika mazingira magumu na zinatakiwa kupambana kujinasua na janga la kuteremka daraja.

Kwa mujibu wa kanuni, msimu ujao timu nne zitashuka moja kwa moja na mbili zitacheza mechi za mchujo. Jumla ya timu sita zitashuka.

Pamoja na mshikemshike huo, wapo mabeki bora wa upande wa kulia ambao hadi sasa wamefanya vizuri wakiwa na timu zao.

Spoti Mikiki inakuletea orodha ya mabeki 10 waliocheza kwa kiwango bora katika nafasi hiyo bila kuangalia timu anayocheza ipo nafasi gani katika msimamo wa Ligi Kuu.

Shomari Kapombe-Simba

Pia Soma

Advertisement
Beki huyo ameendelea kulinda kiwango chake na amekuwa chachu ya mafanikio ya Simba katika mechi za msimu huu.

Kapombe akiwa na msimu wa tatu tangu aliporejea Simba amezidi kuwa bora kutokana na uwezo wake wa kupiga krosi akiwa ndiye mwanzilishi wa mashambulizi akitokea upande wa kulia.

Juma Abdul-Yanga

Msimu uliopita chini ya kocha Mwinyi Zahera, Abdul alikosa namba kikosi cha kwanza baada ya kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara.

Majeraha hayo yalimuibua beki chipukizi Paul Godfrey ‘Boxer’ ambaye alikuwa chaguo la kwanza. Hata hivyo baada ya beki huyo kuumia, Abdul alirejesha namba na haikushangazwa kuitwa timu ya Taifa ya Bara iliyoshiriki mashindano ya Cecafa nchini Uganda.

Mwaita Gereza-Kagera Sugar

Ingawa si chaguo la kwanza kwa kocha Mecky Maxime kwa kuwa nafasi hiyo anatumika zaidi Ally Salum, lakini Gereza amekuwa moto.

Hata hivyo, Gereza ameonyesha kiwango bora katika mechi alizocheza. Uwezo wake ulitoa nafasi kwa benchi la ufundi la timu ya Taifa ya Bara kwenda naye katika mashindano ya Cecafa.

Nico Wadada-Azam

Beki huyo raia wa Uganda amejihakikishia namba katika kikosi cha Azam, Wadada amekuwa katika kiwango bora tangu alivyofika nchini na hakuwahi kuchuja.

Uwezo wake umemfanya awe mmoja wa wachezaji waliocheza mechi nyingi katika mashindano msimu huu.

Datius Peter-Mbao

Licha ya kwamba huu ndio msimu wake wa kwanza kucheza Ligi Kuu, kinda huyo ameonyesha uwezo mkubwa akiwa na kikosi cha Mbao.

Ni beki bora katika kuzuia mashambulizi na uwezo wake mzuri unaweza kumuondoa Mbao katika usajili wa msimu ujao.

Mizar Kristom-Namungo

Achana na Reliant Lusajo au Lucas Kikoti, Namungo yupo beki chipukizi anaitwa Mizar ambaye amekuwa mhimili katika safu ya ulinzi.

Licha ya kutokuwa na jina, jicho la kocha Juma Mgunda lilitua kwa Kristom ambaye alimuita timu ya Taifa ya Bara kwa mashindano ya Kombe la Cecafa. Kinda huyo atakuwa bora endapo ataendeleza makali yake kwa misimu michache ijayo akipata uzoefu.

William Lucian-Namungo

Wengi wanamfahamu kwa jina la Gallas. Hajawahi kuchuja uwezo wake tangu akiwa na Simba. Ni mmoja wa mabeki wachache waliolinda vyema vipaji vyao.

Mashabiki wa soka wanamuita Gallas akifananishwa na nahodha wa zamani wa Arsenal, William Gallas aliyekuwa mmoja wa mabeki bora Ufaransa.

Duchu Emmanuel-Lipuli

Msimu huu umekuwa mzuri kwake baada ya kucheza mechi takribani zote tangu ajiunge na timu hiyo.

Duchu ni miongoni mwa mabeki wa kulia wanaofanya vizuri katika mechi za Ligi Kuu.

Kibwana Shomari-Mtibwa Sugar

Hili ni zao la Mtibwa Sugar la muda mrefu mpaka anakwenda katika kikosi cha timu za vijana Taifa. Mwaka jana akiwa katika Kombe la Mapinduzi alionyesha kiwango bora.

Ubora wake umemfanya kocha Zuberi Katwila kumuamini na kumpa namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza.

Kelvin Kijili-KMC

Tangu alivyoumia Boniface Maganga, Kijili alijihakikishia namba ya kuanza katika kikosi cha kwanza.

Beki huyo ameonyesha uwezo akitumia nguvu na akili kuvaana na mawinga machachari wenye kasi uwanjani. Haitashangaza Kijili akisajiliwa na klabu kongwe msimu ujao.

Chanzo: mwananchi.co.tz