Wakati Michuano ya Kombe la Dunia ikiendelea nchini Qatar, Makala hii inekuletea wachezaji watano waliocheza mechi nyingi za Michuano hiyo, na rekodi hizi huenda zikabadilika pale tu michuano ya mwaka huu itakapofika tamati.
5.DIEGO MARADONA-ARGENTINA
Mkongwe huyu ni Moja Ya wachezaji Bora kuwahi kutokea ulimwenguni alifanikiwa kucheza michezo 21 Ya mashindano haya na magoli 8. Mwaka 1986 alishinda kiatu cha dhahabu na kombe la Dunia, Fundi huyu amewahi kuwa kocha wa Timu Ya taifa Ya Argentina pia.
4.UWE SEELER-GERMAN
Amechezo michezo 21 Ya mashindano haya na kufunga magoli 9, Aling'ara zaidi katika kombe la Dunia mwaka 1958. Ni miongoni mwa wachezaji waliocheza michezo mingi zaidi katika michuani hio mfululizo.
3.PAULO MALDINI-ITALY
Beki huyu kitasa wa Azzuri amecheza michezo 23 Ya Kombe la Dunia na kufunga magoli 3. Ni miongoni mwa mabeki bora kuwahi kutokea Duniani kutokana na umahiri na ubora wake sambamba na Kariba Ya Uongozi. Aling'ara zaidi kombe la Dunia mwaka 1990 italy.
2.MIROSLAV KLOSE- GERMAN
Mshambuliaji huyu, Amecheza mechi 23 za mashindano hayo na ndio mfungaji bora wa muda wote wa mashindano hayo akiwa na magoli 16. German Target Man ana rekodi kibao katika mashindao hayo kutokana umahiri wa kucheza na kufunga magoli.
1.LOTHAUR MATTHAUS -GERMAN
Gwiji huyu ndio kinara akiwa amecheza mechi 25 za kombe la dunia, Umaarufu wake ulitokana na umahiri mkubwa na 1990 alishinda kombe hilo na Ballon D'or . Ni moja Ya wachezaji waliocheza Michuano Hio mara tano tangu mwaka 1982-98 bila kukosa.