Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hawa ndio Manahodha wanatakaoongoza Mataifa yao Qatar

Manahodha Messi na Ronaldo

Tue, 18 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ni miongoni mwa manahodha watakaowakilisha timu zao za taifa katika fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Qatar kwa mara ya kwanza mwezi ujao.

Mastaa hawa licha ya kuwa manahodha wa timu zao za taifa hawana historia ya kubeba ubingwa wa Kombe la Dunia licha ya kupata mafanikio mengi katika ngazi ya klabu.

Ronaldo ana umri wa miaka 37 huku mpinzani wake akiwa na umri wa miaka 35. Kwa upande wa Messi ametangaza rasmi fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Qatar mwaka huu zitakuwa za mwisho kwake. Lakini kwa upande wa Ronaldo bado hajaweka wazi hilo.

Kwenye orodha hii yupo Hugo Lloris mwenye historia ya kubeba taji hilo akiwa na kikosi cha Ufaransa mwaka 2018, vilevile yupo Robert Lewandowski anayewakilisha Poland, staa huyu amepata mafanikio ngazi ya klabu alipokuwa akikipiga Bayern Munich kabla ya kujiunga na Barcelona dirisha la usajili la kiangazi mwaka huu.

Hawa hapa manodha 32 watakaowakilisha mataifa yao kwenye fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Qatar.

1. Mathew Ryan (Australia, Real Sociedad)

2. Ehsan Hajsafi (Iran, AEK Athens)

3. Maya Yoshida (Japan, Sampdoria)

4. Hassan Al-Haydos (Qatar,Al Sadd)

5. Salman Al-Faraj (Saudi Arabia, Al-Hilal)

6. Son Heung-min (South Korea, Tottenham)

7. Vincent Aboubakar (Cameroon,Al Nassr)

8. Andre Ayew (Ghana,Al Sadd)

9. Romain Saïss (Morocco, Wolves)

10. Kalidou Koulibaly (Senegal, Napoli)

11. Youssef Msakni (Tunisia, Al Duhail)

12. Atiba Hutchinson (Canada, Besiktas)

13. Bryan Ruiz (Costa Rica, Alajuelense)

14. Andres Guardado (Mexico, Real Betis)

15. Christian Pulisic (Marekani, Chelsea)

16. Lionel Messi (Argentina, PSG)

17. Thiago Silva (Brazil, Chelsea)

18. Enner Valencia (Ecuador, Fenerbahce)

19. Diego Godin (Uruguay, Velez Sarsfield)

20. Eden Hazard (Ubelgiji, Real Madrid)

21. Luka Modric (Croatia, Real Madrid)

22. Simon Kjaer (Denmark, AC Milan)

23. Gareth Bale (Wales, Los Angeles FC)

24. Harry Kane (England, Tottenham)

25. Hugo Lloris (Ufaransa, Tottenham)

26. Manuel Neuer (Ujerumani, Bayern Munich)

27. Virgil van Dijk (Uholanzi, Liverpool)

28. Robert Lewandowski (Poland, Barcelona)

29. Cristiano Ronaldo (Ureno, Manchester United)

30. Dusan Tadic (Serbia,Ajax)

31. Sergio Busquets (Hispania, Barcelona).

32. Granit Xhaka (Uswisi, Arsenal).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live