Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hawa kazini kwao kuna kazi

Kibwana Yao Yanga Hawa kazini kwao kuna kazi

Sat, 26 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ligi Kuu Bara inazidi kuchanja mbuga kwa michezo kadhaa kupigwa kwa baadhi ya timu lakini balaa lipo kwa wachezaji wapya wanavyopewa nafasi na kuonesha kiwango kikubwa.

Dirisha hili la usajili baadhi ya timu ziliingiza maingizo mapya na katika baadhi ya mechi zilizochezwa wachezaji hao wameanza kuonyesha matokeo mazuri.

Wachezaji hao wapya kama wakiendelea kuonyesha viwango vizuri basi hata wale wa zamani watakuwa na kazi kubwa ya kuwaaminisha walimu wa timu hizo kuwa wana kiwango bora.

Katika timu za Simba, Yanga, Azam FC na Singida Fountain Gate kuna baadhi ya sajili zimeonekana kulipa kutokana na kile kilichokitarajiwa na mashabiki na viongozi wa timu hizo.

 Lakini ubaya upo kwa wale wa zamani ambao kama wakibweteka kidogo tu basi wageni wanachukua nafasi ya kikosi cha kwanza moja kwa moja.

Mwanaspoti linakuletea baadhi ya wachezaji wapya watakaowapa wa zamani changamoto kupata namba katika kikosi cha kwanza.

1.Tchakei v Bruno- Singida FG

Moja kati ya sajili ambazo zinaonekana kulipa ni kwa kiungo mshambuliaji, Marouf Tchakei raia wa Togo aliyejiunga na Singida Fountain Gate msimu huu akitokea AS Vita Club ya DR Congo kwa mkataba wa miaka miwili.

Tangu amejiunga na Singida, Tchakei ameonekana kuingia moja kwa moja kwenye mfumo wa Kocha Hans Pluijm na kama ataendelea kuonyesha kiwango bora, basi ni wazi atachukua nafasi ya Bruno Barroso aliyekuwa kikosini hapo tangu msimu uliopita.

Ingizo la Tchakei kikosini hapo limeanza kukonga nyoyo za mashabiki wa timu hiyo kutokana na kile ambacho ameanza kukionyesha.

Kiungo huyo mpaka sasa amecheza mechi tatu mbili za Ngao ya Jamii  dhidi ya Simba ambapo iliondoshwa kwa penalti 4-2 na dhidi ya Azam ilipofungwa mabao 2-0 na JKU ilipoondoka na ushidi wa mabao 4-1 kwenye Kombe la Shirikisho Afrikahatua ya awali.

Kwenye mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Azam Complex Chamanzi Tchakei alihusika na kufunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao manne.

Kiwango chake hakitofautiani sana na Mbrazili, Bruno ambaye amekuwa na uwezo wa kuunganisha timu na kuipa faida ya mabao lakini pia amekuwa akiisaidia kuzuia.

2.Pacome v Azizi KI- Yanga

Safu ya kiungo mshambuliaji ya Yanga ni eneo ambalo lina ushindani mkali. Kikosi hicho kilichocheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita chini ya Nasreddine Nabi aliyetimkia AS Far Rabat ya Morocco.

Msimu uliopita kulikuwa na vita katika eneo hilo ambapo alikuwa Feisal Salum ‘Feitoto’ aliyehamia Azam FC na kwasasa vita imerudi kwa Azizi na Pacome.

Aziz hakuwa na mwendelezo mzuri kwani hakupata nafasi ya kucheza kwa dakika zote 90 na msimu huu ameanza kuonesha makali yake kwa kutupia bao moja moja katika mashindano mawili.  Akifanya hivyo kweye mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC ambapo Yanga ilishinda mabao 2-0 na katika mechi ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika iliposhinda 2-0 dhidi ya Asas FC ya Djibout.

Pacome kwenye mechi dhidi ya Asas aliingia dakika ya 61 na kuonyesha kiwango bora ambacho kama Aziz atazembea mchezaji huyo bora wa Ligi ya Ivory Coast anaweza kumwandoa kikosini.

3.Yao v Kibwana- Yanga

Baada ya aliyekuwa beki wa kulia, Mkongomani, Djuma Shaban kuwa na uhusiano mbaya na viongozi na benchi la ufundi, Yanga ikaamua kuingia sokoni na kumleta Yao Atohoula kutoka Asec Mimosas ya Ivory Coast.

Beki huyo ni miongoni mwa majina yanayosifika nchini kwa kuonesha kiwango bora na kumfanya tangu Kocha Miguel Gamondi aanze kumtumia katika mechi tatu hajamuweka benchi.

 Yao amekuwa bora na kubeba matumaini makubwa kwa Wanajangwani kwenye eneo hilo ambalo pia hucheza na Kibwana Shomari na Nickson Kibabage aliyesajiliwa msimu huu akitokea Singida Fountain Gate.

Yao ambaye pia anacheza kama winga amesajiliwa msimu huu lakini anaonesha upinzani mkali hasa eneo hilo ambalo anacheza dakika zote 90.

Ubora wa beki huyo unampa hatihati ya kukosa namba katika kikosi cha kwanza Kibwana ambaye katika mechi tatu hakupata nafasi ya kuingia hata dakika moja kukitumikia kikosi hicho.

4.Ngoma v Kanoute- Simba

Msimu uliopita, Sadio Kanoute ndiye aliyekuwa anaongoza kwa kuwa na kadi nyingi za njano katika kikosi cha Simba.

Alimaliza na kadi 10 na kama Fabrice Ngoma ataonesha kiwango bora basi huenda staa huyo wa Mali asipate nafasi ya kuitumikia Simba kama ilivyokuwa.

Wakati Ngoma akitumia mbinu laini kuwadhibiti washambuliji na viungo wa timu pinzani hali hiyo ni tofauti kabisa na Kanoute ambaye uchezaji wake ni mgumu na  umekuwa ukimfanya apate kadi nyingi za njano na mara nyingine nyekundu.

Kiungo huyo kama hatabadilika msimu huu atapata changamoto kutoka kwa Ngoma ambaye ni ingizo jipya la msimu huu akitokea Al Hilal ya Sudan. Licha ya hivyo, tangu amerudi uwanjani msimu huu hajawa katika ubora wake kama ule aliokuwa nao msimu uliopita.

Ni jambo la muda tu kama  atashindwa kuonesha kiwango kizuri basi kuna uwezekano akashindwa kucheza katika kikosi cha kwanza.

Pia, Ngoma ni mchezaji mwenye uwezo wa kucheza sehemu nyingi uwanjani na mara kadhaa ameonekana akicheza kama beki wa kati, ingawa muda mwingi hucheza kiungo wa juu na ana uwezo wa kufunga pia.

Ametua Simba kwa mkataba wa miaka miwili na kama ataonyesha vitu vyake vya ziada anaweza kumpa presha Kanoute.

Erick Johora v Sebusebu Samson- Geita Gold

Tangu kipa Erick Johora ajiunge na Geita Gold amepindua nafasi ya Sebusebu aliyekuwa anacheza kama kipa namba moja wa timu hiyo.

Johora kabla ya kujiunga na Geita alitokea Yanga ambako hakupata nafasi zaidi ya kucheza Kombe la Mapinduzi msimu uliopita, tofauti na makipa waliokuja nyuma yake kama  Aboutwalib Mshery na Metacha Mnata ambao angalau walipata nafasi mbele ya namba moja, Djigui Diarra.

Baada ya kusajiliwa Geita na sasa amecheza mechi mbili za Ligi Kuu na kuondoka na ‘Cleansheet’ mbili kama ataendelea kuboresha kiwango chake na kuwa na mwendelezo basi ni wazi namba moja ataikamata na kumpora namba Sebusebu.

Kalolanya v Benedict Haule-Singida FG

Singida imemsajili Beno Kakalonya akitokea Simba na wadau wengi waliamini anaenda kuwa Mfalme Kwa Walima Alileti hao, lakini mambo yameonekana kuwa magumu mbele ya Benedict Haule ambaye yupo na timu hiyo tangu msimu uliopita.

Kakolanya ametumika kwenye mechi mbili tu za Ngao ya Jamii, lakini hakacheza katika Kombe la Shirikisho Afrika wala kwenye ligi kuonyesha kuna upinzani mkali katika kupambania namba mbele ya mwenyeji wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live