Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hawa hapa Mastaa wa Singida watakaoikosa Yanga Ijumaa hii

Mastaa Singida Hawa hapa Mastaa wa Singida watakaoikosa Yanga Ijumaa hii

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipa wa Singida Big Stars, Beno Kakolanya anatarajia kuukosa mchezo wa Ligi dhidi ya Yanga Ijumaa Oktoba 27.

Kakolanya hakuwa sehemu ya mazoezi ya kikosi hicho yaliyofanyika leo Uwanja wa Gymkhana tayari kwa ajili ya mchezo huo.

Singida Big Stars inatarajia kuwa mgeni wa Yanga kwenye mchezo huo ambao ni wa saba kwa timu zote mbili huku wenyeji wakiwa vinara wa msimamo wakiwa na pointi 15 na SBS wakiwa nafasi ya saba kwenye msimamo baada ya kukusanya pointi nane.

Mbali na Kakolanya mastaa wengine ambao wanatarajia kukosekana kwenye mchezo huo ni Joash Onyango, Thomas Ulimwengu na Hamad Waziri 'Kuku'.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya SBS kililiambia Mwanaspoti kuwa Kakolanya aliumia kisigino kwenye mchezo dhidi ya Namungo, Onyango, Ulimwengu na kuku pia ni majeruhi.

"Wachezaji wote ambao hawajaonekana kwenye uwanja wa mazoezi ni majeruhi lakini wengine wote wapo fiti," anasema.

Alipoulizwa Ofisa Habari wa SBS, Hussein Massanza alisema ni kweli hawajaonekana kwenye uwanja wa mazoezi lakini haina maana kwamba hawapo kwenye mipango ya mwalimu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: