Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hawa KMC ni Azam watupu

KMC Vs Yanga Jamhuriii Hawa KMC ni Azam watupu

Sat, 17 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kikosi cha KMC kimecheza mchezo wa Ligi Kuu Bara leo dhidi ya Ynga katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro huku kikosi chake cha kwanza kikiwa na sura ya Azam FC nyuma yake.

Kwenye kikosi cha kwanza cha KMC kina watu 9 waliowahi kupita Azam FC huku watano wakianza kikosi cha kwanza dhidi ya Yanga.

KMC ilianza na kipa Wilbol Maseke, viungo Issah Ndala, Awesu Awesu na washambuliaji Shaban Chilunda na Waziri Junior ambao waliwahi kuitumikia Azam FC.

Kwenye benchi lao walikuwa na wachezaji wawili beki Ismail Gambo na winga Tepsie Evance pamoja na makocha wawili, Abdihamid Moalin na msaidizi wake John Matambala ambao waliwahi kufanya kazi pamoja Azam.

Sio hao tu bado Azam Iia damu yao kwa wachezaji wawili walikuwa jukwaani kiungo Masoud Cabaye na kinda beki Twalib Nuru.

Kwenye wachezaji hao ni wawili pekee ambao wako KMC kwa mkopo Ndala na Nuru huku wengine wote wakiwa ni wachezaji halali wa timu hiyo.

Chanzo: Mwanaspoti