Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Havertz anaitaka Namba 9 Arsenal

Kai Havertz Goal Kai Havertz

Mon, 3 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Staa, Kai Havertz amesema kwamba anachofahamu yeye ni Namba 9 wa Arsenal baada ya kunogewa na kile alichokifanya kwenye Ligi Kuu England kwa msimu wa 2023-24.

Staa huyo wa kimataifa wa Ujerumani, Havertz, 24, alijiunga na Arsenal akitokea Chelsea kwa ada ya Pauni 65 milioni kwenye dirisha la uhamisho wa majira ya kiangazi la mwaka jana.

Licha ya kwamba awali kocha Mikel Arteta alimnasa staa huyo kwa mipango ya kuja kucheza kwenye sehemu ya kiungo, Havertz alibadilishiwa majukumu na kuchezeshwa kama straika.

Havertz, ambaye amechangia mabao 20 kwenye Ligi Kuu England, ikiwa tisa kwenye mechi 14 za mwisho wakati wa mbio za ubingwa, amemaliza msimu akiwa mchezaji wa tatu kwa mabao kwenye kikosi hicho cha Arsenal chenye maskani yake Emirates.

Na sasa, Havertz anaamini ataendelea kutumika kwenye nafasi hiyo ya Namba 9 kwa msimu ujao.

Havertz alisema: “Najiona mwenyewe kama Namba 9 kwenye timu ya taifa na sasa kwenye kikosi cha Arsenal. Lakini, sina maana kama Namba 9 wa viwango. Wachezaji wa hivyo wako wapi? Hata Erling Haaland au Harry Kane, ambao wakati mwingine hawaonekani kubaki tu kwenye boksi ili wafunge.

“Wachezaji wanaosubiria kwenye boksi kwa sasa hawapo kwenye soka. Mimi ni mtu ninayefurahia kushambulia na kurudi nyuma. Na nafahamu kwamba kila kitu kitahitaji mabao yangu.”

Havertz amezungumza hilo baada ya kuwapo kwa ripoti kwamba Arsenal ipo kwenye hatua za mwisho kumsajili straika Benjamin Sesko aje acheze Namba 9.

Chanzo: Mwanaspoti