Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Hatutaki maneno maneno kwa Wachezaji wetu"- bumbuli

Yanga Sc Media Officer Hassan Bumbuli Spge0rsmuoel148ictakf1pod?fit=1200%2C800&ssl=1 Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Yanga, Hassan Bumbuli

Tue, 28 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Juzi wakati wa mechi ya Ngao ya Hisani kati ya Simba na Yanga, kuna tukio lilitokea kati ya mchezaji wa Yanga Yannick Bangala ambapo alimuonesha kidole cha kati kumuelekea mchezaji wa Simba.

Picha za video zinamuonesha Bangala akifanya kitendo hicho ambapo wachambuzi mbali mbali wa msuala ya mpira nchini wamekiongelea wakitaka mamlaka zichukue hatua.

Sasa Mkuu wa kitengo cha Habari klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli ameibuka na kudai wachezaji wao waachwe na hao wanaojiita wachambuzi.

Bumbuli amesema kwa wachezaji yapo mengi yanayotokea uwanjani na ndio maana mwisho wa mchezo wanashikana mikono na kukumbatiana na kama kuna kosa ni lile ambalo lipo katika ripoti ya mwamuzi

"Kuna tabia ya watu wanaojiita wachambuzi kuleta "choko choko" kwa wachezaji wetu, wanaropoka sijui midomo ya flani imetamka hiki na hiki, sisi tunasema watuache"

"Hawa wanapishana vingi wakiwa uwanjani kwa hiyo wanayamaliza wenyewe ndani ya uwanja wewe wa nje huku hayakuhusu, wasilete ujuaji kwa wachezaji wetu" amesema Bumbuli

Wakati huo huo Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amesema wakati wa kunyamaza hivi sasa umekwisha, na hakuna mudsa wa kucheka na wale wasioitakia mema klabu ya Yanga.

Kauli hiyo ni kama fumbo kwenda kwa mchambuzi wa michezo wa kituo cha redio ya E-fm, Jemedari Said ambae amelizungumzia muda mwingi sana tukio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live