Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatushuki, Ihefu yatamba

9d6a50e04da8d7c4e9adb68a0df5713f Hatushuki, Ihefu yatamba

Mon, 29 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KOCHA Mkuu wa Ihefu, Zuberi Katwila amesema ana imani kubwa kikosi chake hakitashuka daraja msimu huu.

Ihefu ni moja ta timu zilizopanda Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu na mwenendo wake si mzuri kwenye ligi hiyo.

Katwila aliyejiunga na timu hiyo katikati ya msimu akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro alisema anajua timu yake iko kwenye wakati mgumu kwa sasa lakini atapambana ibaki Ligi Kuu.

Ihefu imecheza mechi 24 na kufikisha pointi 20 pekee ikiwa nafasi ya 17 kwenye msimamo wa ligi hiyo yenye timu 18.

Katwila aliliambia gazeti hili jana kuwa bado kuna mechi kadhaa kabla ya kumalizika kwa ligi, anaimani atazitumia hizo kujiweka sawa na kuhakikisha timu yake inacheza Ligi Kuu msimu ujao.

“Ni kweli tupo kwenye wakati mgumu, lakini haimaanishi kwamba hatuna uwezo wa kupambana kubaki Ligi Kuu, tutabaki naamini,” alisema.

Aliwataka mashabiki wa Ihefu kutokata tamaa bali wawape sapoti.

“Wakati huu ni muhimu kwa mashabiki wetu kutoa sapoti yao kwa timu kwani wachezaji wanawahitaji sana,” alisema.

Alisema ligi imezidi kuwa ngumu hasa inapoelekea mwishoni maana hakuna timu inayotaka kushuka daraja.

“Kila timu inapambana kwa sasa isishuke daraja na hapo ndipo ligi inapozidi kuwa ngumu, lakini sisi tutapambana na nashukuru wachezaji wangu wana ari kubwa,” alisema.

Chanzo: www.habarileo.co.tz