Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatukusajili kwa video clip - Try Again

Try Again Pic Hatukusajili kwa video clip - Try Again

Wed, 30 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Klabu ya Simba SC, Salum Abdallah 'Try Again' amesema usajili walioufanya msimu huu, ulizingatia mahitaji yao na si kutumiwa clip za wachezaji.

Try Again amefunguka hilo kupitia Simba APP ambapo ameweka wazi kuwa, kabla ya kusajili waliangalia malengo kwa msimu huu mpya na ndipo walipoingia kusaka nyezo za kufikia malengo yao.

"Malengo yetu ni kuchukua mataji yote ya ndani lakini pia kuvuka robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika, nyezo tulizokuwa tunahitaji ni wachezaji na benchi zuri la ufundi. Tuliwatafuta wachezaji ambao wanacheza kwenye timu zao, wengine ni ma-MVP kwenye timu zao lakini wengine ni ma-top scoler kwenye timu zao.

"Hatukusajili tu kwa kuangalia clip za kwenye mitandao, wengine tuliwafatilia wakiwa wanacheza bila hata wao wenyewe kujua kama mnavyofahamu tuliajiri kitengo maalum cha skauting," alisema Try Again.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live