Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatukati tamaa ya ubingwa- Kaze

A3cb92f1d730eec682fef61b6317987e.jpeg Hatukati tamaa ya ubingwa- Kaze

Tue, 16 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

KOCHA wa Yanga, Cedric Kaze amesema licha ya vikwazo vingi wanavyofanyiwa na waamuzi hawawezi kukata tamaa ya kupigania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Kaze alitoa kauli hiyo akimlalamikia mwamuzi Ludovic Charles wa Tabora aliyechezesha mchezo wa timu yake na Mbeya City uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.

Akitoa tathimini baada ya kumalizika kwa mchezo huo uliokuwa mgumu, Kaze alidai kuwa na waamuzi wasio na ubora inakatisha tamaa na inapunguza ushindani kwa timu.

Alisema maamuzi ambayo aliyafanya dakika ya 90 na kuwazawadia Mbeya City mkwaju wa penalti, iliyofungwa na Pastor Atanas,yalikuwa ovyo hivyo kuendelea kufanya hivyo ni kuwaamiza wachezaji.

“Hatuwezi kuwa na ligi inayovutia kama waamuzi watakuwa wanatoa maamuzi kama haya, sijui kama kunamtu aliona kama mchezaji alinawa mpira eneo la hatari,”alisema.

Pia alisema pamoja na matokeo hayo hawawezi kukata tamaa na wanajipanga kwa mchezo unaokuja wa ligi dhidi ya Kagera Sugai uliopangwa kuchezwa kesho kutwa Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Naye kocha wa Mbeya City Mathias Lule alisema pointi moja kwao kutoka kwa Yanga ni matokeo mazuri na wanajipanga kwa mchezo ujao dhidi ya Azam FC kuhakikisha wanafuta makosa.

“Mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa nawapongeza wachezaji wangu kwa pointi moja kutoka kwa Yanga na tunajipanga kwa mchezo unaokuja kuhakikisha tunapata matokeo mazuri,”alisema Lule.

Matokeo hayo yanawafanya Yanga kuendelea kuongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 45 kwa michezo 19 waliyocheza huku Mbeya City wakisalia nafasi ya 17 kwenye msimamo baada ya kucheza michezo 19.

Chanzo: habarileo.co.tz