Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatma ya Sakho, Wawa leo Simba SC

Wawa Pic Data Hatma ya Sakho, Wawa leo Simba SC

Mon, 27 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

HATMA ya kiungo mshambuliaji, Ousmane Sakho na beki Pascal Wawa na wenzao watatu itajulikana leo, ya kuendelea au kubakia kukipiga Msimbazi.

Wachezaji hao ndiyo wanaotajwa kuachwa katika usajili wa dirisha dogo kwa ajili ya kupata nafasi za kusajili wa kigeni.

Nyota wengine wanaotajwa kuachwa katika timu hiyo ni kiungo, Duncan Nyoni, kipa Jeremiah Kisubi, na kiungo mkabaji Abdoulswamad Kassim.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo tumezipata, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Muhispania Franco Pablo leo Jumatatu anatarajiwa kukabidhi ripoti ya usajili.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa ripoti hiyo atakayoikabidhi ndiyo itakayoamua wachezaji wa kuachwa na kusajili ambao amewapendekeza katika dirisha dogo.

Aliongeza kuwa mara baada ya ripoti hiyo kukabidhiwa kwa Bodi ya Wakurugenzi, haraka uongozi utachukua maamuzi ya kutangaza wachezaji wa kuwaacha na kuwasajili.

“Kesho (leo) kila kinachohusiana na usajili kitajulikana mara baada ya kocha kutukabidhi ripoti ya usajili katika usajili huu wa dirisha dogo.

“Ripoti hiyo ndiyo itakayoamua wachezaji wa kuachwa na kusajili wapya baada ya tetesi nyingi za usajili kusambaa katika vyombo vya habari,” alisema mtoa taarifa huyo.

Simba kwa kupitia Mshauri wa Bodi wa Wakurugenzi ya Simba, Crescentus Magori ilisema: “Ni kweli hatujapata ripoti ya usajili ya kocha hadi hivi sasa, lakini tunatarajia kuipata Jumatatu (leo) baada ya kutoka Tabora kucheza dhidi ya KMC.

“Baada ya kuipata ripoti hiyo, bodi itakutana kujadili na kuchukua maamuzi ya usajili wa wachezaji wapya ambao kocha amewahitaji pamoja na wa kuachwa.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live