Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatma ya Pamba na wenzake kujulikana leo

Pamba+pic Hatma ya Pamba na wenzake kujulikana leo

Tue, 21 Jul 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Yohana ChalleHATUA ya mwisho ya hatua ya mtoano kwa timu zinazoshuka daraja Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zinachezwa leo Jumanne kwa viwanja viwili kuwaka moto.

Boma FC ambayo katika mchezo wa kwanza ilichapwa 2-1 dhidi ya Mawenzi Market itakuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Kipija, Mbeya kuwakaribisha wapinzani wao.

Kocha Mkuu wa Boma FC, Muhibu Kanu anasema bao moja walilolipata ugenini linawapa nguvu kwenye mchezo huo ili kuhakikisha inapata ushindi na kubaki FDL.

"Tunajua mchezo utakuwa mgumu kwa timu zote mbili maana kila mmoja anahitaji ushindi au sare kwa upande wa wenzetu ambao walipata ushindi kwaoi," amesema Kanu.

Mchezo mwingine wa leo, Pamba FC itakuwa nyumbani kuikaribisha Friends Rangers kwenye kipute kitakachopigwa Uwanja wa Nyamagana, Mwanza.

Katika mchezo uliopita timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1, mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz