Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatma ya Muandaaji wa AFCON 2027 kujulikana leo

Ndumbaro CAF Hatma ya Muandaaji wa AFCON 2027 kujulikana leo

Wed, 27 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uamuzi mkubwa na muhimu unaohusu hatima ya Tanzania na mataifa mengine mawili kutoka Afrika Mashariki kuandaa michuano ya Kombe la Afrika 2027 utafahamika leo Jumatano.

Tanzania imeungana na Kenya na Uganda kuwasilisha ombi walilolibatiza jina la ‘Pamoja Bid’ wakiwa na matumaini kwa mara ya kwanza ukanda wa Afrika Mashariki utaandaa michuano hiyo mikubwa ya soka.

Kwa Kenya itakuwa ni mara ya pili inajaribu kuomba kuwa mwenyeji baada ya ombi la kwanza 1996 kukubaliwa, lakini baadaye wakapokonywa na kuhamishiwa Afrika Kusini.

Mwaka 2017, Kenya waliomba tena kuwa mwenyeji lakini safari hii michuano ya Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa ndani (CHAN) ombi ambalo pia lilikubaliwa ila kwa mara nyingine tena wakapokonywa na michuano hiyo kuhamishiwa Rwanda.

CAF pia inatarajiwa kutaja taifa litakaloandaa Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 kutokana na Guinea kupoteza sifa Oktoba mwaka jana baada ya kubainika taifa hilo lililo Magharibi mwa Afrika lilikuwa nyuma ya wakati kwenye maandalizi ya michuano hiyo itakayoshirikisha mataifa 24.

Mataifa yanayowania kuwa mwenyeji wa Afcon 2025 ni Algeria, Morocco, Zambia na muunganiko wa Benin na Nigeria, wakati Pamoja Bid inatunishana misuli kuwa mwenyeji Afcon 2027 dhidi ya Algeria, Botswana na Misri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live