Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatma ya Mbisa Prisons ni leo

Mbisa Pic Data Mussa Mbisa

Mon, 12 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatima ya kipa wa Tanzania Prisons, Mussa Mbisa kurejea uwanjani imeanza kutoa matumaini akisubiri majibu ya kipimo cha mwisho leo Jumatatu ili kuanza mazoezi mepesi.

Kipa huyo alisajiliwa kutokea Coastal Union ambapo katika michezo 15 ya mzunguko wa kwanza amecheza mechi moja tu ambapo pia hakumaliza dakika 90 alipoumia wakati wa mchezo dhidi ya Singida Big Stars.

Tangu hapo nyota huyo aliyewahi kung’ara na Mwadui amekuwa nje akiuguza jeraha la mguu ambapo imeelezwa kuwa katika vipimo vya daktari ilionyesha kuna mifupa midogo ilivunjika kwa ndani.

Mbisa alisema kwa sasa yapo matumaini kwani maendeleo yake siyo mabaya na anasubiri kipimo cha mwisho Jumatatu ili kujua lini aanze mazoezi mepesi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live