Mason Greenwood hakujumuishwa katika kikosi kizima cha Manchester United msimu huu na taarifa kuhusu hatima yake itatolewa hivi karibuni.
Straika huyo mwenye umri wa miaka 21 alipigwa ‘stop’ kuichezea timu hiyo Januari, mwaka jana kufuatia kesi ya tuhuma ya udhaliishaji na ubakaji na hakushiriki shughuli zote zinazohusu klabu hiyo.
Greenwood alishtakiwa kwa jaribio la kutaka kubaka, kushambulia na kutishia kuua kabla ya mashtaka kufutwa Februari, mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa huenda mkataba wake ukavunjwa au kutolewa kwa mkopo ama kuuzwa huku AS Roma na Atalanta zikihusishwa.
Hivi karibuni Greenwood alinaswa na kamera akifanya mazoezi akiwa amevaa jezi ya timu ya taifa ya Jamaica akisubiri uamuzi kuhusu hatima yake. Wakati hayo yakiendelea kocha Erik ten Hag na wachezaji wenzake wanataka arudi kwenye timu.
Kabla ya sakata hilo kumkabili Greenwood alikuwa amefunga mabao 35 katika mechi 129 alizocheza.