Dar es Salaam. Kocha Luc Eymael hafurahishwi na hali ya kukosekana kwa weledi katika Ligi Kuu Tanzania Bara, hatma ya kuendelea kuwa Yanga itategemea na majadiliano yake na mkewe.
Mbelgiji huyo alisaini mkataba wake wa miezi 18 na Yanga mapema Januaria baada ya kuachana na Black Leopards. Hata hivyo katika mkataba wake una kipengele cha kuvunja mkataba baada ya miezi sita.
Eymael alianza vizuri, lakini sasa mambo yamebadilika na kushuhudia timu yake ikipata sare nne mfululizo na kuporomoka hadi nafasi ya nne katika msimamo wa ligi.
"Angalia hii, angalia kiwanja tulichochezea Jumanne iliyopita na vyumba vya kubadilishia nguo. Nilitakaa wachezaji wangu wasiingie huo," alisema Eymael huku akionyesha picha hizo lakini kwa bahati mbaya hazikuweza kufungua ili kuonekana.
Eymael aliuambia mtandao wa KickOff.com kuwa alilazimika kuwaambia wachezaji wake wabadilishie nguo kwenye basi na kwenda kukaa katika viti vya plastiki uwanjani.
Eymael alisema hana uhakika kama ataendelea kubaki Tanzania msimu ujao.
Pia Soma
"Kwa kweli sijui... lakini... mazingira ya hapa ya kipekee. Sijawahi kukutana na changamoto nyingi kama hizi kwa wakati moja. Nitajadiliana na mke wangu juu ya suala hili."Nina uzoefu wa miaka 10 katika bara lenu... lakini hapa... sijawahi kukutana na hali kama hii. Lakini natakiwa kuendelea kuwepo, kwa sababu sina uchaguzi."
Eymael pia amelalamikia ratiba ngumu ya Ligi Kuu Tanzania katika mwezi wa Februari akicheza mechi kila baada ya siku tatu.
"Angalia ratiba yetu kuanzia Februari 2. Ni mara sita ya ile ya Boxing Day England. Mbaya," alisema Eymael. "Viwanja vipo juu, lakini ratiba ngumu kweli..."
Ratiba ya Yanga kwa Februari:
Ruvu Shooting Stars vs Yanga SC - 08/02
Yanga SC vs Mbeya City - 11/02/20
Yanga SC vs Tanzania Prisons - 15/02
Police Tanzania vs Yanga SC - 18/02
Coastal Union vs Yanga SC - 23/02
Yanga SC vs Gwambina - 26/02
Yanga SC vs Alliance FC - 29/02