Hatma ya golikipa wa klabu ya Manchester United raia wa Hispania David de Gea ipo matatani kwani taarifa zinaeleza kua huenda akatimka klabuni hapo katika dirisha hili kubwa.
Kumekua na mazungumzo ya muda mrefu baina ya klabu na golikipa huyo juu ya kuongeza mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia mashetani hao wekundu, Lakini De Gea mpaka sasa hajakubaliana na Manchester United juu ya ofa ambayo imemuwekea mezani.
Taarifa za ndani zinaeleza kua golikipa huyo alieitumikia klabu hiyo kwa muda mrefu amepiga chini ofa ya mkataba mpya ya klabu hiyo, Huku sababu zikielezwa ni maslahi ambayo yapo kwenye mkataba huo mpya na hayajampendeza golikipa huyo kwani anahitajika kupunguza mshahara wake ili kusalia klabuni hapo.
David Dea Gea ndio mchezaji anaelipwa zaidi ndani ya klabu ya Manchester United hivo kupewa ofa ya mkataba mpya ambayo itamuhitaji kupunguza maslahi yake ni kitu ambacho inaelezwa hajakubaliana nacho kabisa, Kutokana na hali hiyo kuna uwezekano mkubwa kipa huyo akatimka ndani ya majira haya ya joto.
Kuondoka kwa De Gea pia kunasababishwa na kubadilika kwa mpira kwani timu nyingi zinahitaji golikipa wa kisasa ambaye anaweza kucheza kuanzia nyuma na kupiga pasi kwa usahihi, Kitu ambacho Mhispaniola huyo hakiwezi na kocha Ten Hag nara kadhaa ameongelea juu ya kuhitaji golikipa mwenye uwezo wa kucheza kuanzia nyuma na mwenye ufanisi katika kupiga pasi.