Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatimaye, mnyama huyoo makundi Kombe la Shirikisho Afrika

Simba Yafuzu Makundi Wachezaji wa Simba wakisalimia mashabiki baada ya mchezo dhidi ya Red Arrows

Sun, 5 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa wa Tanzania, Simba SC wamefanikiwa kufuzu Hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika licha ya kuchapwa mabao 2-1 na wenyeji, Red Arrows jioni ya leo Uwanja wa Taifa wa Mashujaa Jijini Lusaka, Zambia.

Mabao ya Red Arrows yamefungwa na Ricky Banda dakika ya 45 na Sadam Phiri dakika ya 48, wakati bao pekee la Simba SC limefungwa na Kiungo Hassan Dilunga dakika ya 67.

Simba SC inaingia hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa 4-2 kufuatia kushinda 3-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumapili iliyopita Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live