Rais wa Klabu ya Yanga SC, Eng. Hersi Ally Said amefanya mahojiano mbalimbali kuhusu wachezaji klabu hiyo na kufafanua mambo mbalimbali likiwemo suala la Kiungo Feisal Salum Abdallah kama akihitajika na klabu itakayotoa dau nono zaidi.
Eng Hersi amesema wanaweza kumshawishi kiungo huyo abaki klabuni lakini kama watazidiwa dau, watamruhusu aondoke.
"Kama tunaweza kumshawishi abaki kwetu atabaki, kama ofa hiyo ni kubwa zaidi na Sisi hatuwezi kuimudu na mchezaji yupo tayari kwenda tunafungua milango."
"Tulimruhusu Tuisila akiwa anapendwa lakini Maono ya uongozi kwenye mpira tunahitaji hivyo na Tuisila alikuwa amebakisha mwaka mmoja, je umbakize aondoke bure au ufungue milango upate pesa na ulete mbadala, maamuzi kama hayo yanatakiwa kufanyika," alisema Eng. Hersi.