Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatimaye TFF kutangaza kocha mpya wa Taifa Stars

Paulsen Stars F Kim Poulsen

Thu, 26 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania [TFF] kupitia kwa Mkurugenzi wa Ufundi Oscar Milambo limesema, litamtangaza Kocha wa Taifa Stars mwanzoni mwa mwezi Februari mwaka huu.

Tangu kuondoshwa kwa Kim Poulsen mwezi Agosti, 2022 hakutangazwa mrithi wake badala yake alitangazwa Honour Janza kukaimu nafasi hiyo lakini pia aliondoka mwishoni mwa mwaka uliopita.

Oscar Milambo kupitia amesema, wanatafuta Kocha anaeendana na mazingira ya nchi yetu ili kuepuka changamoto walizokutana nazo miaka iliyopita.

“Tupo kwenye huo mchakato wa kutafuta Kocha wa Timu ya Taifa na mchakato unaendelea, muda si mrefu sana tutaujuza umma tumefikia wapi na ni nani tunafikiri anaweza kuchukua hayo majukumu.”

“Tunafahamu na tayari tunaushahidi kwamba tumeshawahi kuwa na walimu na nini pengine kilisababisha hatukufikia malengo tuliyokuwanayo kama Shirikisho na kama nchi.”

“Tunajaribu kufanya hesabu vizuri ili mwalimu tutakaemtangaza tuwe tumejiridhisha kwamba hatutakutana na changamoto ambazo tumepitia siku za nyuma.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live