Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatimaye Simba wamtambulisha Saido Ntibanzokiza

Simbasctanzania~p~Cmi Z8Vs19s~1 Hatimaye Simba wamtambulisha Saido Ntibanzokiza

Sat, 24 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Usajili wa dirisha dogo unazidi kutikisa nchini baada ya dirisha dogo kufunguliwa rasmi Desemba 15, 2022. Wekundu wa Msimbazi Simba SC, wamtambulisha rasmi Kiungo Mshambuliaji raia wa Burundi, Saido Ntibanzokiza.

Kupitia ukurasa wao, Simba wametupia picha ya nyota huyo aliyekuwa akiitumikia Geita, na kumtambulisha kama mchezaji wao mpya.

Saido ataungana na mastaa wengine wa Simba kama Clatous Chama, Moses Phiri, Agustine Okrah, Pape Sakho na wengineo kuongeza nguvu katika eneo la ushambuliaji.

Simba wamesema wanatarajia kuongeza wachezaji wawili au watatu kwenye dirisha dogo linalotarajiwa kufungwa Januari 15, 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live