Kocha wa timu ya Taifa ya DR Congo, Sébastien Desabre leo Jumanne ameita kikosi cha timu hiyo na kuwajumuisha wachezaji wanaokipiga Tanzania, Fiston Mayele wa Yanga na Henock Inonga wa Simba.
Desbare raia wa Ufaransa amekiita kikosi hicho cha wachezaji 42 huku Mayele na Inonga wakiwa ni wachezaji pekee wa DR Congo wanaocheza Ligi Kuu NBC kuitwa na kocha huyo.
DR Congo imeita kikosi hicho kwa ajili ya maandalizi ya mechi mbili za kufuzu michuano ya Mataifa Afrika (Afcon 2023) dhidi ya Mauritania zitakazopigwa Machi 24 na marudiano Machi 29, mwaka huu.
Kuitwa kwa wachezaji hao ambao wamekuwa wakionesha viwango bora tangu watue nchini kumekuja wakati ambao wachezaji hao wametoka kuzisaidia timu zao kupata pointi kwenye mechi za makundi Ligi ya Mabingwa Afrika wikiendi iliyopita.
Mayele ambaye anaitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi hicho tangu atue Yanga misimu miwili iliyopita, alifunga bao kwenye sare ya 1-1 dhidi ya Real Bamako ya Mali na kuifanya Yanga iondoke na pointi moja ugenini.
Mayele ndiye kinara wa mabao katika Ligi Kuu ya Tanzania kwa msimu huu mpaka sasa akiwa na mabao 15. Msimu uliopita Mayele alimaliza akiwa wa pili na mabao 16 nyuma ya mfungaji Bora, George Mpole aliyekuwa Geita Gold akiwa na mabao 17.
Tofauti na Mayele, Inonga amekuwa akiitwa katika kikosi hicho mara kwa mara kwenye kikosi hicho.
Inonga alifunga bao pekee kwenye ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Vipers ya Uganda na kuipa Simba pointi tatu za kwanza msimu huu kwenye michuano hiyo baada ya awali kufungwa bao 1-0 na Horoya ya Guinea na kisha kuchapwa mabao 3-0 na Raja Casablanca ya Morocco.
DR Congo imeita makipa watano, mabeki 13, viungo 16 na washambuliaji wanane wakitazamiwa kupunguzwa kabla ya kufikia maandalizi ya mwisho mwisho dhidi ya mechi na Mauritania.
KIKOSI CHA AWALI KILICHOITWA;
WALINDA MILANGO:
B. SIADI
E. KABAMBA
J. KIASSUMBUA
L. MPASI
H. LOMBOTO
WALINZI:
D. MUKOKO
G. KALULU
J. IKOKO
S. M'BAKATA
A. MASUAKU
J. KAYEMBE
V. N'SIMBA
A. ZOLA
C. MBEMBA
H. BAKA✅
L. IKOYO
M. BOKADI
P. OUANEH
VIUNGO
A. TSHIBOLA
E. KAYEMBE
P. RUDDOCK
S. BASTIEN
T. MUYUMBA
M. MICHE
C. KINSOMBI
J. OKITA
M. ELIA
M. LILEPO
T. BONGONDA
A. LUSAMBA
S. MOUTOUSSAMY W. BALIKWISHA
G. DIANGANA
C. AKOLO
WASHAMBULIAJI:
C. BAKAMBU
F. MAYELE✅
G. LAURA
J. MULEKA
S. KATOMPA
G. KAKUTA
A. KALULU
Y. WISSA.