Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatimaye Maxi Nzengeli amejitafutra, amejipata!

Zx Maxi Mudathir Hatimaye Maxi Nzengeli amejitafutra, amejipata!

Fri, 9 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Maxi Mpiah Nzengeli baada ya ulame wa mabao kwa takribani mechi 10 alizocheza, hatimaye amefanikiwa kufunga bao lake la nane kwenye Ligi Kuu ya NBC.

Magoli ya Maxi Nzengeli na Mudathir Yahya, yameifanya timu ya Young Africans SC kuendelea kutanua kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kufikisha pointi 37 jana Februari 8, 2024.

Hiyo ni baada ya Young Africans SC kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Mashujaa FC katika mchezo wa ligi hiyo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Maxi alikuwa wa kwanza kufunga goli dakika ya 44, kabla ya Mudathir Yahya kuongeza la pili dakika ya 85.

Ushindi huo unaifanya Young Africans SC kuzidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo na kuiacha Azam FC inayofuatia nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi 6.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live