Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatimaye De Gea apata timu

David De Gea Record David De Gea

Sat, 10 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kipa wa zamani wa Manchester United, David de Gea ameripotiwa kufikia makubaliano ya kujiunga na Fiorentina kwa mkataba wa mwaka mmoja. Inaelezwa.

Kipa huyo wa kimataifa wa Hispania amekuwa nje ya uwanja kwa mwaka mmoja sasa tangu aachane na Man United katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana.

Amekuwa katika mazungumzo na baadhi ya timu za Saudi Arabia na Ulaya lakini hakuna hata moja iliyowahi kufanikiwa kumshawishi kabla ya Fiorentina kufanikisha hilo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari Fabrizo Romano De Gea amefanya makubaliano binafsi na mabosi wa Fiorentina na atajiunga na timu hiyo ndani ya siku chache zijazo.

Awali staa huyu alikuwa akihusishwa kuwa huenda angetua Genoa kabla ya dili kufeli katika dakika za mwisho kutokana na masuala ya kimslahi.

Kipa huyu aliyewahi kuahidiwa mshahara wa karibia Pauni 500,000 kwa wiki na Al Nassr anataka kuendelea kucheza soka la kushindani barani Ulaya na hitaji lake la mshahara ni Pauni 5 milioni ambayo Genoa iliona nyingi.

Akiwa na Man United aliyoitumikia kwa misimu 12, staa huyu alicheza mechi 545 za michuano yote na alikuwa mmoja kati ya mastaa wanaokunja pesa nyingi na kwa wiki alikuwa akichukua Pauni 375,000.

Katika mkataba huo wa mwaka mmoja na wanafainali hao wa michuano ya Europa Conference League kuna kipengele cha kuuongeza kwa mwaka mmoja zaidi ikiwa ataonyesha kiwango bora.

Kwa mujibu wa ripoti De Gea mwenye umri wa miaka 33, atasafiri kwenda Italia kufanya vipimo vya afya kabla ya kusaini dili hilo.

Fiorentina ambayo inashiriki michuano ya Conference Leagu inaweza kumpa De Gea ya kukutana na waajiri wake wake wa zamani, Man United ikiwa watashushwa kutoka Europa League.

Kwa sasa timu kutoka England anayoweza kukutana nayo ni Chelsea pia inashiriki michuano hiyo.

Mchezo wake wa kwanza unatarajiwa kuwa Agosti 17 na Fiorentina itacheza dhidi ya Parma siku ya kwanza ya msimu mpya wa Serie A.

Chanzo: Mwanaspoti