Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatimaye Chama Afunguka Kurejea Tanzania

Luis Chama Pic Data Hatimaye Chama Afunguka Kurejea Tanzania

Wed, 1 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

HATIMAYE aliyekuwa kiungo wa Simba, Clatous Chama ameamua kufunguka kuhusu kurejea Tanzania huku ikidaiwa kuwa mazingira ya Morocco yamemshinda.

"Kuna mambo mengi ninayakumbuka hapo Tanzania, maana niliishi na viongozi na wachezaji wa Simba SC vizuri, hata mashabiki nao niliishi nao vizuri, kuna mambo mengi sana ninayakumbuka kwa kweli.

"Kuhusu mchezaji ambaye ninamkumbuka sana ni Shomari Kapombe, kwa sababu tuliishi chumba kimoja tukiwa kambini Simba SC, kuna mengi sana ambayo ninamkumbuka Kapombe, pia ninawakumbuka wachezaji wengine wa klabu ya Simba na viongozi pia.

"Siwezi kusema lolote kuhusu kurudi Tanzania, kwa sasa mimi ni mchezaji wa RS Berkane, sina budi kujizatiti katika majukumu yangu kwenye klabu hii," Clatous Chama, Kiungo RS Berkane.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live