Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatimaye Bellerin arejea Barcelona

Hector Bellarine.jpeg Hector Bellerin

Sat, 3 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hector Bellerin, 27, amekamilisha uhamisho wa  kwenda Barcelona kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kudumu Arsenal kwa muda wa miaka 11.

Beki huyo ameondoka Arsenal kwani hakuwa katika mipango ya Mikel Arteta msimu huu, licha ya kurejea kwa mkopo Real Betis, alipokuwa akikipiga.

Bellern alikuwa amebakiza mkataba wa mwaka mmoja Arsenal lakini baada ya makubaliano na mabosi beki huyo alipewa ruhusa ya kuondoka na kusitisha mkataba wake.

Ikumbukwe kuwa, Bellerin alikulia katika kituo cha kukuza vipaji La Masia (Catalunya) tangu alipokuwa na umri wa miaka16. beki huyo aianza kuichezea Arsenal tangu mwaka 2013, amecheza jumla ya mechi 250, na kubeba makombe matatu ya FA pamoja na Ngao ya Jamii.

"Leo tunamuaga Hector na tunamshukuru sana kwa uaminifu wake na mchango wake Arsenal, kwa pamoja tumetengeneza historia nyingi ndani na nje ya uwanja tunamtakia kila kheri katika maisha yake mengine mapya" alisema Mikel Arteta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live