Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatimaye Azam FC yavunja ukimya kumtaka Kocha Moalin

Kocha KMC Moalin.jpeg Hatimaye Azam FC yavunja ukimya kumtaka Kocha Moalin

Thu, 2 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Azam imekana tetesi za kwamba inahitaji huduma ya aliyewahi kuwa kocha wake Mkuu, Abdihamid Moalin 'Master Lecturer' ambaye kwa sasa anakiona kikosi cha KMC.

Kupitia mitandao ya kijamii, Ofisa Habari wa Klabu ya Azam, Hasheem Ibwe ameandika hayo kufuatia tetesi hizo zinazohusishwa na Azam FC kutaka kuachana na kocha wake, Yousuf Dabo kutokana na matokeo mabovu ya kikosi hicho.

"Of course Moalin ni Kocha Mzuri na tunaheshimu uwezo wake pia tunawaheshimu waajiri wake KMC, lakini hayupo kwenye mpango wowote wa kurejea Azam FC na hakuna mazungumzo yoyote ambayo yamefanyika wala mjadala ndani ya team kuhusu kocha huyo.

"So Puuzieni hizo hadithi ni madalali tu wanaopambana na kivuli cha Kocha wetu Dabo," amesema Ibwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live