Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Hata wakiondoka, Simba haiwezi kutetereka" - Kibaden

Wanaondoka.jpeg Nyota wa simba wanaotajwa kuwaniwa na Vigogo wa Soka Afrika

Thu, 12 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa zamani wa Machampioni wa nchi, Abdallah Kibadeni amesema Klabu ya Simba ni klabu kubwa na haiwezi kutetereka kwa kuondokewa na nyota wake wawili wanaozungumzwa kuhitajika na baadhi ya Vilabu nje ya Nchi.

Akihojiwa na kituo cha redio cha Wasafi Fm, cha Jijini Dar es Salaam, Kibadeni amefunguka namna ambavyo klabu ya Simba haiwezi kufanya makosa na kuwashusha presha mashabiki wa klabu hiyo.

"Hatua waliyoifikia Simba hivi sasa wako vizuri, wanachokiamua chochote ni sahihi na wana mipango" amesema King Mputa.

"Hapa Simba wanaangalia suala la biashara, hivyo mashabiki wasiwe na wasi wasi, benchi la ufundi litatafuta mbadala sahihi na wana uzoefu wa kujua nini wanachokihitaji" ameeleza king Mputa.

Kwa takribani wiki mbili sasa kumekua na tetesi juu ya kuhitajika kwa nyota wawili wa klabu ya Simba na Vigogo wa soka barani Afrika. Luis Miquissone ambae anahitajika na Al-Ahaly ya Misri na wakati huo huo Clatous Chama anahitajika nchini Morocco.

Ofa ambayo imetolewa kwa wachezaji hao ni zaidi ya bilioni tatu, hivyo inaonekana ni ngumu simba kukataa, na tayari wameshaanza kufanya baadhi ya sajili kitu kinachoonekana kama ni kuziba mianya itakayoachwa na nyota hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live