Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hata inyeshe vipi, watapigwa tu!

Simba X Yanga 1 Hata inyeshe vipi, watapigwa tu!

Sun, 5 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zege halilali. Ndivyo unavyoweza kusema, kuelekea mchezo wenye mvuto zaidi nchini, Simba SC vs Yanga SC maarufu Kariakoo derby, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Saa 11:00 jioni.

Licha ya mvua kushamiri katika Jiji la Dar es Salaam, Bodi ya Ligi Kuu nchini (TPLB) imewatoa hofu wapenzi wa mpira wa miguu kwa kuandika kupitia ukurasa wao wa Instagram "Hata inyeshe vipi lazima kitapigwa #KariakooDerby"

Simba SC ni mwenyeji katika mchezo huo nambari 111, tangu wakutane kuanzia miaka 1960's.

Matokeo chanya kwa timu moja wapo kati ya hizi mbili, yataisogeza hadi kileleni mwa msimamo wa Ligi.

Hadi sasa, wote wana points 18. Yanga, ipo mbele kwa mchezo mmoja, imeshacheza michezo 7 huku Simba ikiwa na michezo 6.

Mchezo wao wa mwisho ulikuwa katika kuwania Ngao ya Jamii, Agosti 13, 2023 katika Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga.

Simba ilishinda kwa changamoto ya penalti 3-1 baada ya dakika 90 kuisha bila mbabe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live