Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hata Yanga kuna N’Golo Kante

Pic+kaseke Hata Yanga kuna N’Golo Kante

Fri, 23 Oct 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

HUKO Jangwani buana kuna N’Golo Kante. Kama hutaki sikia hii. Winga Deus Kaseke amebatizwa jina jipya na wachezaji wenzake wa Yanga ambapo kwa sasa anaitwa jina la nyota wa Kifaransa anayekipiga Chelsea, N’Golo Kante.

Habari ndio hiyo, unaambiwa licha ya kwamba Kaseke ameonekana kutofurahia jina hilo, ila limekaa mdomoni mwa Mukoko Tonombe ambaye amekuwa akipenda kulitumia wakati wa mazoezi kambini kwao Kigamboni.

Kutokana na mazingira ya utani yaliyopo baina wachezaji kwa wachezaji hata na viongozi muda mwingine, Kaseke huishia kutabasamu.

Inaelezwa kupachikwa kwa Kaseke jina hilo kumetokana na nyota huyo wa Yanga kufanana urefu na Kante, huku wote wakiwa wachakarikaji uwanjani utofauti wao ni kwenye nafasi wanazocheza.

Licha ya kwamba muda mwingine kucheza kama kiungo.

 

Chanzo: mwanaspoti.co.tz