Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hat-trick zatawala ASFC

Hat Trick ASFC Hat-trick zatawala ASFC

Mon, 12 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Zikiwa zimebaki mechi mbili tu kukamilisha nafasi za kufuzu hatua ya 32 bora Kombe la Azam (ASFC) rekodi ya Hat-trick imetawala.

Hadi sasa ni Hat-trick sita zimefungwa na mastaa mbalimbali wa ligi kuu huku staa wa Ihefu FC, Adrew Sinchimba akitupia kambani mabao matano timu yake ikiibuka na ushindi wa 9-0 dhidi ya Mtama Boys.

Hat-trick hizo ni kwa wachezaji Richardson Ng’ondya (Mbeya City) mabao manne alifunga kwenye mchezo dhidi ya Stand FC timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 5-1, wakati Moses Phiri (Simba) alimjibu kwa kutupia mabao manne dhidi Eagle FC timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 8-0.

Kama haitoshi, Ihefu FC nao wakicheza kwa ubora waliisambaratisha Mtama Boys mabao 9-0 huku Andrew Simchimba akitakata kwa kutupia matano.

Nyota wa KMC, Sadala Lipangile alitupia mabao manne katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Uhuru dhidi ya Tunduru Korosho timu yake ikiibuka na ushindi wa 6-1.

Ismail Mgunda wa Tanzania Prisons aliiwezesha timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 7-1 dhidi ya Misitu huku yeye akitupia mpira kambani mara tatu.

Mchezaji mwingine ni Clement Mzize (Yanga) aliyefunga mabao manne wakati kikosi hicho kikiibuka na ushindi wa mabao 8-0 dhidi ya Kurugenzi FC.

Mbali na Hat-trick hizo, lakini pia kipa namba tatu wa Yanga, Erick Johora amepata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza kwani mara ya mwisho alicheza dhidi ya Azam FC kwenye mashindano ya Mapinduzi Januari 10 mwaka jana akiingia dakika ya 90 kuchukua nafasi ya Aboutwalib Mshery na kushindwa kuisaidia timu yake kutinga hatua na fainali kwa kufungwa kwa penati 9-8 baada ya timu hizo kutoka suluhu ndani ya dakika 90.

Chanzo: Mwanaspoti