Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hat-trick yampa chips, kuku

Chipsi Kuku Hat Trick Hat-trick yampa chips, kuku

Fri, 17 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Bosi wa timu ya Mwamposa FC, Feisal Musa ametoa ofa ya chipsi na kuku kwa mfungaji wa mabao matatu, Timotheo Elius.

Ilikuwa katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Bodaboda FC uliofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Chang’ombe jijini hapa ambapo Elius alifunga mabao hayo na kuiwezesha timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 4-1.

Mchezo huo ulikuwa mkali na wa kusisimua ambapo tajiri huyo alikuwa akishangilia mwanzo mwisho huku kila mchezaji wake alipokuwa akipiga chenga alikuwa akitoa ahadi ya kununua kitu.

“Mpige chenga nikununulie bodaboda, mpige kanzu mshamba huyo, mpige tobo miguu kama mti, funga hao niwatoe kwenye umaskini wachezaji wangu,” alikuwa akisema bosi huyo pindi mchezaji wake akipiga chenga.

Bosi huyo ambaye ni mmiliki wa banda la Chipsi eneo la Chang’ombe alisema sababu ya kufanya hivyo ni kutokana na kuukubali uwezo wa mchezaji huyo.

“Utakula kuku, chipsi na soda umefanya kazi kubwa, umewafunga mdomo wale bodaboda wenye kelele kila siku,” alimweleza mchezaji huyo mara baada ya filimbi ya mwisho.

Kwa upande wa mchezaji huyo, alisema hiyo ni zawadi nzuri kwake na ataendelea kuuwasha moto katika michezo atakayoichezea timu hiyo.

Chanzo: Mwanaspoti