Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hat trick ya Baleke yaipa jeuri Simba

Jean Baleke MTIBWA 1140x640 Baleke aipa jeuri Simba

Wed, 15 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya juzi Jumamosi, straika Jean Baleke kuibeba Simba kwa kuifungia mabao matatu ‘hat trick’ dhidi ya Mtibwa Sugar, benchi la ufundi la timu hiyo kupitia kwa Kocha Msaidizi, Juma Mgunda umetamba kuwa straika ni miongoni mwa wachezaji hatari na wanataka kuona anacheza kwenye kiwango hicho dhidi ya Horoya.

Baleke juzi Jumamosi alifunga hat trick yake ya kwanza akiwa na Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa kwenye mechi walishinda mabao 3-0. Baada ya mechi hiyo Simba walifikisha pointi 57 na kuendelea kusalia nafasi ya pili ya msimamo.

Simba Jumamosi hii wanatarajia kuwa wenyeji wa Horoya AC ya Guinea katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Mkapa kuanzia saa 1:00 usiku.

Akizungumza nasi, Mgunda alisema: “Tumefurahishwa na namna ambavyo kikosi chetu kilicheza mchezo wetu dhidi ya Mtibwa Sugar na kufanikiwa kupata pointi tatu muhimu lakini pia tumefurahishwa na kiwango alichoonyesha Baleke.

“Ni miongoni mwa washambuliaji bora kwenye kikosi chetu, lakini unajua hivi karibuni alishindwa kufunga katika mechi kadhaa na kwa kiasi fulani ni kama alipoteza kujiamini, tulikaa naye chini na tunaamini ataendelea kuonyesha kiwango bora kuelekea mechi zijazo ikiwemo mchezo dhidi ya Horoya Jumamosi.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live