Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hat-trick Bara sasa mambo yamebadilika

Baleke Aziz Hat-trick Bara sasa mambo yamebadilika

Mon, 25 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Soka ni mchezo unaopendwa na watu wengi zaidi duniani, mchezo huu umekuwa kipenzi kwa kuwahauna matokeo ambayo ni rahisi kuyatabiri. Wengine wanadiriki kusema soka ni mchezo wa kikatili kwani timu yenye kupewa mata-rajio makubwa ya kushinda hujikuta ikifumuliwa na timu inayochukuliwa poa.

Zipo timu vigogo maarufu duniani zimekutana na aibu ya kufungwa mabao mengi kwenye mchezo mmoja na timu zisizotarajiwa. Kumbuka ile 7-2 iliyopewa Liverpool kutoka kwa Aston Villa katika Ligi Kuu ya England au Manchester United kufungwa mabao 6-2 na Tottenham Hotspur miaka ya karibuni.

Pia, kuna vipigo vingine kama vile ya Arsenal ilipofumuliwa 8-2 na Manchester United katika EPL msimu wa 2011/2012, Manchester City ilipochapwa 8-1 na Middleborough mwaka 2008 na hivi karibuni tu msimu wa 2019/2020 Barcelona ilichapwa 8-2 na Buyern Munich kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kifupi kwenye soka kuna maajabu mengi na burudani za ku-sisimua na kati ya vitu vingi ambavyo ni maarufu kwenye soka vinavyotokea ni pamoja na mchezaji kupewa heshima na kuonekana kuwa amefanya jambo kubwa katika mchezo mmoja iwe kwa kuupiga mwingi ama kufunga mabao mengi.

Mojawapo ni wachezaji ambao wamekuwa wakifunga mabao matatu kwenye mchezo mmoja ‘hat- trick’.

Hawa wamekuwa wakitajwa kuwa mastaa kwenye mchezo husika, lakini wakiimbwa kwa kuwa ni jambo ambalo ni nadra sana kutokea kwenye  mchezo huo.

Pamoja na ugumu wa kufunga idadi hiyo ya mabao, lakini kuna wanaume wanashikilia rekodi ya kufunga hat trick nyingi kwenye maisha ya soka, Erwin Helmchen raia wa Uje-rumani hadi sasa anashika nafasi ya kwanza kwa wanasoka waliofunga hat trick nyingi akiwa ametupia 141, huku Pele akiwa amefunga hat trick 92.

Hapa kwetu kwenye Ligi Kuu Bara, rekodi ya hizi karibuni zi-naonyesha mchezaji mwenye hat trick nyingi ni Amissi Tambwe aliyezifunga akiwa na klabu za Simba na Yanga kwa misimu sita kati ya saba aliyodumu kucheza nchini tangu 2013. Mwamba huyo katika misimu hiyo amefunga hat- trick sita tofauti ndani ya misimu hiyo, akifuatiwa na Emmanuel Okwi, Obrey Chirwa na Meddie Kagere waliofunga kati ya hat trick nne na tatu mtawalia kati ya 2017 hadi leo hii.

Rekodi zinaonyesha katika Ligi Kuu Bara msimu uliozalisha hat trick nyingi ulikuwa ni uliopita wa 2022-2023 zilipofungwa tisa, ikiupiku ule wa 2019-2020 uliokuwa na hat trick nane, kisha upo wa 2018-2019 wenye hat trick sita na 2017-2018 ukiwa na nne kama ilivyo kwa sasa kwenye Li-gi ya msimu huu.

Suala la kufunga hat trick limekuwa likitokea kwa nadra, lakini kwa msimu huu limeonekana kuja kwa kasi sana am-bapo wachezaji wanne wameshafunga hat trick kwenye michezo kadhaa waliyocheza, huku ligi ikiwa ndio kwanza inatafuta kumaliza duru la kwanza.

Mchezaji wa kwanza kufanya hivyo ni Feisal Salum ‘Fei Toto’ wa Azam FC, lakini yupo Kipre JR pia wa timu hiyo hiyo, Stephane Aziz Ki ambaye ni kiungo wa Yanga pamoja na mshambuliaji wa Simba, Jean Baleke.

Katika orodha hiyo, jambo kubwa la kujifunga ni kuwa ni mchezaji mmoja tu amefunga hat trick akitokea kwenye eneo la ushambuliaji ambaye ni Baleke.

AINA YA HAT TRICK

Kwenye soka hat trick zimegawanywa katika sehemu kuu mbili, kuna ile ya kawaida, lakini nyingine yenye heshima kubwa zaidi inaitwa ‘Perfect hat-trick’, hii ni ile ambayo mfungaji anafunga bao moja kwa mguu wa kulia, moja mguu wa kushoto na moja kwa kichwa.

HAT TRICK LIGI KUU

Misimu kadhaa nyuma kumekuwa na malalamiko makubwa kuhusu mchezaji anayefunga hat trick kwenye Ligi Kuu Bara kutopewa zawadi yake ya mpira halali wa mchezo kama kanuni inavyosema.

Imewahi kutokea msimu uliopita ambao baadhi ya wachezaji walipewa mipira mbele ya kamera lakini baadaye wali-pokonywa wakiwa vyumbani kwa madai kuwa mipira ni michache.

Saido Ntibazonkiza ni mmoja kati ya wachezaji ambao wali-lalamika msimu uliopita kwa kutopewa mpira baada ya kufunga mabao matatu kwenye moja ya msimu huo.

“Kuna ishu moja tu ya msimu uliopita ambayo ilitokea kwa mchezaji Saido wa Simba ambaye alifunga nikasikia kuwa al-ipewa mpira uwanjani lakini baadaye ukachukuliwa kwa ma-dai kuwa FA walikuwa hawana mipira ya kutosha, hili liliku-wa kosa na tulilifanyia kazi.

“Kikanuni mchezaji anatakiwa kupewa mpira ambao ume-tumika kwenye mchezo, suala la mipira michache haliwezi kumzuia mchezaji anayestahili kupewa zawadi yake, msimu huu kila mmoja amepewa kulingana na kanuni inavyosema,” alisema Afisa Habari wa Bodi ya Ligi Kuu Bara, Karim Boimanda.  

INAVYOTAKIWA

Utaratibu wa sehemu nyingi duniani unaonyesha kwamba mchezaji anayepiga hat trick, anatakiwa kupewa mpira ule uliotumika kwenye mchezo husika.

Kwetu wakati mwingine jambo hilo limekuwa likishindikana kwa kuwa taarifa zinasema bodi ya ligi imekuwa ikivipa vyama vya mikoa mipira mitano, ile inayotakiwa kutumika kwenye ligi kwa msimu husika, hivyo huwa ngumu mchezaji kupewa mpira akifunga kwa kuwa vyama hudai kuwa mipira ni michache.

Lakini wakati mwingine timu hutumia mipira yao kwenye mechi zao, mfano unaweza ukawa unachezwa mchezo wa Yanga vs Kagera, uwanjani inaweza kuwepo mipira 20, kumi ya Yanga, mitano ya Kagera na mitano ya chama cha soka cha mkoa.

Changamoto hutokea baada ya mechi kumalizika halafu mchezaji akafunga mabao matatu ‘hat trick’ kwenye mchezo huo.

Yanga haiwezi kukubali kuachia mpira wake apewe mchezaji kama hatoki kwenye timu yao, kwa kuwa wanafahamu kuwa idadi ya mipira yao itapungua na hakuna sehemu ambayo inasema kwenye kanuni ikitoa mpira wake utarudishwa.

Hali hiyo ipo pia kwenye upande wa chama cha soka cha mkoa, nao ni hivyo hivyo wanakuwa na mipira mitano nao wanahofia kuwa wakiitoa itawachukua muda mrefu kupata mwingine, jambo hili limekuwa likiwafanya wafikiri mara mbili na ikitokea mchezaji amepewa mpira na mwamuzi uwanjani, watumie akili ya kuuchukua kwa maelezo kwamba atapewa na Bodi ya Ligi.

VITUKO SASA

Ni kweli bodi wakati mwingine imekuwa ikiitoa mipira hiyo, lakini inakuwa siyo uhalisia wa hat trick kwa kuwa mpira unaotolewa ni mpya ambao haukutumika kwenye mchezo husika.

“Mchezaji wetu (jina tunalificha) tumekwenda wenyewe kumnunulia mpira, kwa kuwa alifunga mabao matatu lakini hakupewa, hivyo tumeenda dukani tumemnunulia mwingine,” kiliwahi kunukuliwa chanzo kutoka kwenye klabu moja kubwa hapa nchini

Mbali na hao, mshambuliaji wa zamani wa Simba, Emmanuel Gabriel ‘Batgol’ aliwahi kusema, kuna wakati alifunga hat trick akaenda kumpokonya mwamuzi mpira baada ya kuona kuwa hataki kumkabidhi hali ya ambayo ilizua mzozo mkubwa.

“Niliwahi kufunga hat trick kwenye mchezo mmoja wa ligi huko nyuma, mwamuzi akawa hataki kunipa mpira wangu nikamfuata na kumpokonya ulizuka mzozo mkubwa lakini baadaye viongozi waliingilia kati kila kitu kikaenda sawa,” alisema Bat Goal.

SASA MAMBO SAFI

Kuonyesha tatizo limemalizika sasa tunakwenda kisasa zaidi tofauti na hali ilivyokuwa awali, wachezaji waliofunga hat trick hadi sasa, hawajalalamika kuhusu kupewa mipira.

Huku kila mmoja, Jean Baleke, Feisal Salum ‘Fei Toto, Kipre’ wakikiri kuwa wameshapewa mipira yao baada ya kufunga hat trick hali ambayo inaonyesha kuwa sasa mambo ni ma-zuri.

“Niishapewa mpira wangu, nilipofunga tu mechi ikamalizika nikapewa kulikuwa hakuna shida wala maswali yoyote,” alisema Fei Toto aliyekuwa mchezaji wa kwanza msimu huu kufunga hat trick kwenye pambano dhidi ya wageni wa ligi, Kitayosce (sasa Tabora United).

Hiyo inaendana na kauli ya Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi Kuu Bara, Karim Boimanda ambaye alipoulizwa kama tatizo ni kama huko nyuma alijibu;

“Waulizeni hata waliofunga watawaambia, hakuna shida kama hiyo msimu huu kila mmoja amefunga hat trick ame-pewa zawadi yake ya mpira uliotumika kwa mujibu wa kanuni,”  alisema.

MIPIRA YENYEWE IKOJE

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lina mkataba na Kampuni ya Uhlsport, ambao pia mipira ya kampuni hiyo inatumika kwenye Ligi Kuu ya Ufaransa, Ligue 1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live