Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Hasta la Vista" Lionel Messi

Lionel Messi Lionel Messi

Fri, 6 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maua hunyauka,Simulizi huisha lakini hata kumbu kumbu pia husahaulika.Na hii ni ishara tosha kuwa siku hazigandi.

Ndiyo kauli unayoweza kuitumia kwa Mshambuliaji na nyota wa klabu ya Barcelona Lionel Andres Messi,ambae baada ya kudumu kwa takribani miongo miwili katika klabu hiyo na sasa anaondoka.

Klabu ya Barcelona imesema mshambuliaji wake nyota, Lionel Messi hatakuwepo klabuni hapo kwa sababu ya vizuizi vya kifedha na utawala.

Messi, 34, amekuwa mchezaji huru tangu Julai mosi mwaka huu, wakati mkataba wake ulipomalizika,Lakini alikua kwenye Majukumu ya Timu ya Taifa.

Raia huyo wa Argentina,likubali kusaini mkataba mpya uliokuwa na kipengele cha kupunguza mshahara, wiki mbili baada ya mkataba wa awali kumalizika.

Lakini hali hiyo ilitegemea zaidi Barca kuuza wachezaji ili kumudu mshahara wake.

"Pande zote mbili zimeelezea kusikitika kutokana na matakwa ya mchezaji na klabu kutotimizwa," ilisema taarifa ya klabu hiyo.

Barcelona imesema Messi alikuwa tayari kuongeza muda kusalia klabuni hapo alipodumu kwa miaka 21 kwa kusaini mkataba mpya siku ya Alhamisi, na kulaumu La Liga kwa kutofanya hivyo.

Taarifa zinasema kuwa tayari Messi alifikia makubaliano ya kukaa na timu hiyo hadi 2026 - lakini La Liga inasema klabu lazima ipunguze mshahara kabla ya yeye na mchezaji yeyote yule mpya kusajiliwa.

Messi ndiye mchezaji anashikilia rekodi ya ufungaji ya muda wote ya Barcelona,na hata Rais wa Barcelona Joan Laporta ahadi yake pindi alipoingia Madarakani ilikua ni kuhakikisha anambakisha nyota huyo katika viunga vya Catalunya.

"Licha ya FC Barcelona na Lionel Messi kufikia makubaliano na nia ya wazi ya pande zote mbili kutia saini mkataba mpya, hii haiwezi kutokea kwa sababu ya vizuizi vya kifedha na kiutawala (kanuni za Ligi Kuu ya Hispania, La Liga)," klabu imesema.

"FC Barcelona inatoa shukrani za kipekee kwa mchezaji huyo kwa mchango wake katika kukuza klabu na inamtakia kila la kheri katika siku zijazo kwenye maisha yake ya binafsi ya soka." Imeongezeka taarifa ya Barcelona.

Lionel Andrés Messi alianza kuichezea klabu ya Barcelona mwaka 2000,ameichezea klabu hiyo ya Hispania michezo778 amefunga magoli 672 na kushikilia rekodi ya mfungaji wa muda wote wa klabu hiyo.Ameshinda mataji 35 akiwa na Klabu hiyo. Mataji 10 ya La Liga.4 ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya,3 ubingwa wa dunia kwa vilabu,7 kombe la mfalme na mengine mengi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live