Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harry Maguire awazodoa mashabiki England

Maguire X Hendo Harry Maguire awazodoa mashabiki England

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: Dar24

Beki wa England, Harry Maguire amesema mashabiki waliomzomea kiungo Jordan Henderson sio mashabiki wa nchi hiyo.

Henderson alizomewa alipotolewa katika ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki kati ya England dhidi ya Australia na alipoingia kwenye ushindi wa 3-1 wa kufuzu kwa Euro 2024 dhidi ya Italia juzi Jumanne.

Nahodha huyo wa zamani wa Liverpool, Henderson alikosolewa kwa kujiunga na Al-Ettifaq ya Saudi Arabia msimu huu wa joto.

“Mashabiki sahihi wa England hawazomei wachezaji,” alisema Maguire na kuongeza: “Usiwazomee wachezaji wanaojitolea maisha yao kucheza na kufanya kila wawezalo kuifanya nchi hii kuwa na kumbukumbu nzuri na kuwa na wakati maalum kwa ajili yao na familia zao.”

Chanzo: Dar24