Nyota wa Manchester United Harry Maguire amekubali ombi la msamaha kutoka kwa mbunge wa Ghana aliyemdhihaki.
"Tutaonana Old Trafford hivi karibuni," beki huyo aliandika kwenye X, iliyoulikana zamani kama Twitter.
Mbunge Isaac Adongo alikuwa akijadili bajeti mwaka jana alipolinganisha usimamizi wa uchumi wa Makamu wa Rais Mahamudu Bawumia na utendaji wa Maguire uwanjani.
Siku ya Jumanne, Bw Adongo alisema alitaka kurekebisha rekodi hiyo na akamsifu Maguire kama "mwanasoka wa kuleta mabadiliko".
Alikuwa "mchezaji muhimu" wa Manchester United, Bw Adongo alisema wakati wa mjadala wa bajeti.
Lakini hakukata tamaa katika ukosoaji wake kwa Makamu wa Rais Bawumia.
"Kuhusu Maguire wetu, sasa yuko IMF, akiwa na kikombe mkononi," aliongeza.
Bw Bawumia ni mkuu wa timu ya serikali ya usimamizi wa uchumi huku Ghana ikikabiliwa na mzozo mkubwa zaidi wa kiuchumi katika miaka mingi iliyopita.