Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harry Maguire ajishtukia Manchester United

Harry Maguire Ajishtukia Manchester United Harry Maguire ajishtukia Manchester United

Wed, 3 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Imeelezwa kuwa nahodha na beki wa Manchester United, Harry Maguire ameingiwa hofu kuhusu namba yake ndani ya kikosi cha England hivyo anataka kuondoka Manchester United kwenda kusaka nafasi ya kucheza kikosi kwanza.

Maguire kwa sasa amekuwa hana nafasi ya uhakika katika kikosi cha kwanza cha Manchester United tofauti na misimu ya nyuma.

Beki huyo amepoteza namba katika kikosi cha kwanza kutokana na makosa yake ya mara kwa mara na zaidi wamekuwa wakitumika Raphael Varane na Lisandro Martinez.

Wawili hao ambao kwa sasa ni majeruhi, Erik ten Hag amekuwa akimpanga Victor Lindelof na Luke Shaw eneo la beki wa kati na Maguire akisubiri.

Maguire yupo tayari kufanya maamuzi ya kuondoka kikosini hapo kwenda kusaka changamoto mpya ilikuwa na uhakika wa kucheza Fainali za Mataifa ya Ulaya ‘Euro 2024’ akiwa na England.

Maguire anataka kuondoka Man United sababu anahofu kuwa anaweza kupoteza nafasi yake ndani ya England sababu amekuwa hana uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza.

Ndiyo maana beki huyo kwa sasa atalazimika kusaka timu mpya ilikuwa na uhakika wa kuitumikia England katika Fainali za Euro 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: