Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harry Maguire aiwekea ngumu Man United

Harry Maguire Akubali Msamaha Kutoka Kwa Mbunge Wa Ghana Harry Maguire

Mon, 15 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Beki wa Manchester United na England, Harry Maguire amewaambia mabosi wa timu hiyo kwamba anataka kubakia katika kikosi na kupambania nafasi yake.

Maguire ambaye alikuwa karibu kuondoka katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana ambapo West Ham ilimwekea ofa mezani, ni mmoja kati ya wachezaji waliokuwa katika mpango wa kuuzwa na Man United kwa ajili ya kukusanya pesa itakazotumia kufanyia usajili.

Staa huyo kwa sasa amerejea mazoezini kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya ambapo kabla ya hapo alifanya mazungumzo na kocha pamoja na viongozi juu ya mustakabali wake na akawaambia kwamba bado anaamini ana nafasi na anataka kubaki.

Alikuwa ni miongoni mwa wachezaji waliorejea mazoezini mapema baada ya kuwa nje kwa muda kutokana na majeraha yaliyosababisha akose hadi michuano ya Euro.

Mkataba wa Maguire unamalizika mwakani na Man United ilikuwa inataka kumuuza ili asije kuondoka bure mwisho wa msimu ujao kwani kocha hajatoa ruhusa ya kuurefusha.

Moja kati ya maeneo ambayo Man United inapambana kuyaboresha kwa sasa ni la beki wa kati ambapo imewaweka katika rada zao Jarrad Branthwaite, na Matthijs de Ligt.

Mazungumzo na Bayern Munich kuhusu mpango wa kumnunua De Ligt, 24, yamekuwa yakiendelea kwa siku kadhaa na ripoti za zimeonyesha kwamba yanaendelea vizuri huku De Ligt mwenyewe akiripotiwa kuwaambia Bayern kwamba anahitaji kuondoka.

Changamoto bado ipo kwa Branthwaite ambaye Everton imeendelea kushikilia msimamo wao wa kuhitaji Pauni 70 milioni.

Man United imetuma ofa mbili ambazo hazijafikia kiasi hicho na zote zimekataliwa.

Chanzo: Mwanaspoti