Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harry Kane hashikiki Ujerumani

Harry Kane Perfect Harry Kane

Sun, 10 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Harry Kane usiku wa jana alifunga hat trick yake ya nne katika Ligi ya Ujerumani (Bundesliga) Bundesliga na kuzidi kuboresha rekodi zake ndani ya klabu ya Bayern Munich anayoitumika kwa msimu wa kwanza.

Kane alifunga mabao hayo wakati Bayern ikiifumua Mainz kwa mabao 8-1 kwenye uwanja wa nyumbani wa Allianz Arena na kupunguza pengo la pointi kati ya timu hiyo na Bayer Leverkusen inayoongoza msimmo wa ligi hiyo kubakia saba, Bayern ikicheza mechi 25 na wapinzani wao mechi 24.

Nahodha huyo wa England amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick nne katika msimu wa kwanza wa Bundesliga, huku mabao 30 aliyoyafunga katika Bundesliga kwa msimu huu yakifikia rekodi ya Uwe Seeler ya kufunga mabao mengi katika msimu wake wa kwanza ndani ya Bundesliga.

Nyota huyo wa zamani wa Tottenham, pia amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga angalau mara mbili katika mechi nane tofauti katika msimu wake wa kwanza wa Bundesliga na sasa kufikisha jumla ya mabao 36 katika michuano yote akiwa na Bayern Munich akiisaka rekodi ya Robert Lewandowski ya kufunga mabao 41 katika msimu mmoja katika ligi hiyo.

Kane amefunga pia mabao sita katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, akiivusha Bayern hadi robo fainali na kwa sasa inasubiri kujua itavaana nani, mbali na kuasisti mara sita katika Bundesliga na tatu za UEFA.

Katika mechi ya jana, Kane alifunga mabao hayo dakika ya 13, 45+7 na 70, huku mengine yakiwekwa kimiani Leon Goretzka aliyefunga mawili dakika ya 20 na 90+2, Thomas Muller (dk 47), Jamal Musiala (dk 61) na Serge Gnabry aliyefunga dakika ya 66 na kuifanya Beyern ifikishe pointi 57, huku Leverkusen ikiwa na 64 na saa 3:30 usiku itashuka uwanjani kucheza mechi ya 25 dhidi ya Wolfsburg.

Chanzo: Mwanaspoti