Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harry Kane atoa kauli nzito, Tottenham waamue kusuka au kunyoa?

Levy X Kane Harry Kane atoa kauli nzito, Tottenham waamue kusuka au kunyoa?

Wed, 9 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Harry Kane amefauhamisha Uongozi wa Tottenham kwamba hataweza kuondoka katika klabu hiyo mara tu msimu mpya wa Ligi Kuu ya Uingereza utakapoanza.

Tayari Kane ameingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake ndani ya Spurs na amekuwa akiwaniwa sana na Bayern Munich kitu ambacho kimeshuhudia ofa tatu zikirudishwa kwa mshambuliaji huyo, ofa ya mwisho ikiwa ni ya rekodi ya klabu yenye thamani ya €100m (£86m).

Bayern walikuwa wamesisitiza kuwa ofa yao ya tatu ndiyo itakuwa ya mwisho kwao lakini inafahamika kuwa wanazingatia mbinu ya nne ambayo inataka kutumiwa na Kane.

Wakati miamba hao wa Ujerumani wakitafuta chaguo lao, imethibitika kwamba Kane ameweka wazi kuwa hatafikiria kuondoka Spurs mara tu msimu mpya utakapoanza wikendi hii.

Spurs wanatazamiwa kumenyana na Brentford tarehe 13 Agosti, ikiwa bado yuko klabuni mpaka tarehe hiyo, basi Kane anapanga kubaki angalau kwa kipindi chote cha msimu, jambo ambalo litamfanya Kane kuweza kuondoka bure msimu ujao.

Spurs wachague kusuka ama kunyoa. Wamuuze Kane kabla ya msimu kuanza au wamuache msimu ujao aondoke bure.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live