Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harry Kane amkosha Antonio Conte

Harry Kane 2 Harry Kane

Fri, 6 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Antonio Conte amemsifia Harry Kane baada kuonyesha kiwango bora kwenye mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Crystal Palace usiku wa kuamkia jana.

Kane alifunga mabao mawili kwenye mchezo huo Tottenham ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0 baada ya kichapo walichopata dhidi ya Aston Villa wikiendi iliyopita.

Ushindi huo unakuwa wa kwanza kwa Tottenham tangu fainali za Kombe la Dunia zilipomalizika Qatar, Kane akikaribia rekodi ya mkongwe wa klabu hiyo Jimmy Greaves baada ya kufunga bao lake la 198 katika mechi 300 alizocheza.

Conte akasisitiza Kane ni straika hatari dunia baada ya kuisaidia Tottenham kupata ushind kwenye mchezo wao wa ligi.

"Tunamuongelea mchezaji hatari kabisa duniani, atavunja rekodi nyingi sana za kufunga mabao, ndio tuna kipindi kigumu, yupo tayari kupambana anapokuwa uwanjani, ana uwezo wa kutoa asisti na kufunga mabao," alisema Conte.

Licha ya ushindi huo Spurs imejikita nafasi ya tano kwa tofauti ya pointi mbili dhidi ya Manchester United kwenye msimamo wa ligi.

Kabla ya mchezo wao dhidi ya Crystal Palace, Conte alitishia ataondoka endapo mabosi wa klabu ya Tottenham hawatamizia mahitaji yake anayohitaji.

"Lengo ni kuipa mafanikio Spurs, kuleta ushindani na kuimarika zaidi, mambo yanvyoendelea kwasasa haya sio malengo ninayotaka,kama nataka kubaki natakiwa kukubali hali halisi, lakini kama sipendezwi basi mlango upo wazi" alisema Conte.

Conte liweka wazi kama Tottenham inataka kuingia katika mbio za ubingwa siku za usoni wanatakiwa kusajili wachezaji hatari kwenye kikosi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live