Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harry Kane aitangazia vita Man United kesho

Skysports Harry Kane Bayern Munich 6265178 Straika wa Bayern Munich, Harry Kane

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Harry Kane kwa mara ya kwanza anarejea kucheza nchini kwao England akiwa na klabu ya Taifa lingine tangu alipoondoka Tottenham Hotspurs mwanzoni mwa msimu huu.

Harry atakutana na Manchester United wakati timu yake ya Bayern Munich itakapokipiga kwenye mchezo wa mwisho wa makundi dhidi ya Manchester United pale Old Trafford.

Bayern anaingia katika mchezo huo akiwa na kumbukumbu mbaya baada ya kupoteza goli 5-1 dhidi ya Eintracht Frankfurt kwenye mchezo wa Ligi huku Man United nayo ikiwa imetoka kupokea kichapo cha goli 3-0 dhidi ya Bournemouth.

Huu ni mchezo mhimu zaidi kwa Manchester United kupata ushindi ili iweze kufuzu kwenda hatua inayofuata ya robo fainali lakini Harry amesema ataenda kuizamisha meli bila huruma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live