Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harry Kane aahidiwa mshahara wa kufuru Spurs

IMG 4487 Levy, Kane.jpeg Harry Kane aahidiwa mshahara wa kufuru Spurs

Wed, 12 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Hotspurs na nahodhawa timu ya taifa ya Uingereza Harry Kane ameahidiwa mshahara wa kufuru kama atakubali kunaki ndani ya klabu hiyo kutoka Kaskazini mwa jiji la London.

Harry Kane ameahidiwa kiasi cha paundi laki tano kwa wiki kama atakubali kusalia na mwenyekiti wa klabu hiyo Daniel Levy, Mshambuliaji huyo amekua mawindo ya vilabu vngi barani ulaya hivo Spurs wanahitaji kutumia nguvu kubwa kumbakiza.

Mshambuliaji huyo anafukuziwa na klabu ya Bayern Munich kwasasa kwa karibu sana lakini Tottenham wanataka kuhakikisha staa huyo anabakia klabuni hapo kwa kumuahidi mshara mkubwa ambao atakua analipwa kuliko mchezaji yeyote ndani ya ligi kuu ya Uingereza.

Harry Kane anahitaji zaidi kupata mafanikio kitu ambacho ndio kinamsababisha kufikiria kuondoka ndani ya Spurs, Kwani mshambuliaji huyo hajafanikiwa kutwaa taji lolote ngazi ya klabu na inaelezwa ndio sababu kubwa ya yeye kutaka kutimka.

Daniel Levy anaamini kua kiwango cha mshahara ambacho amemuekea mchezaji huyo kitaweza kumbakiza ndani ya timu hiyo, Lakini vyanzo vinaeleza kuia tatizo la Harry Kane sio pesa bali anahitaji kushinda mataji zaidi kitu ambacho ndani ya Spurs hakioni kikitokea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live