Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harry Kane: Kustaafu bado sana

Kane England Euros Scaled Harry Kane: Kustaafu bado sana

Thu, 18 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mshambuliaji wa Bayern Munich na England Harry Kane amesema ameumizwa sana na kukosa taji la Euro mbele ya Hispania wiki iliyopita lakini atajipanga upya na bado ana muda mrefu wa kuitumikia England.

Kupitia ujumbe mrefu wenye maneno 84 katika ukurasa wake wa instagram, Kane ambaye alidaiwa kuwa huenda angestaafu kucheza soka la kimataifa baada ya alisema anajipanga kwa ajili ya michuano mingine ijayo.

"Tumevunjika moyo hatukuweza kufikia kile tulichokifanyia kazi kwa bidii, ilikuwa michuano mirefu na migumu, hivyo najivunia kuona tulifika fainali, hivyo licha ya kushindwa kutimiza lengo letu, hili pia ni la kujivunia."

"Hakuna namna zaidi ya kusimama na kujitoa mavumbi na kuwa tayari kuipigania tena jezi ya England, asanteni mashabiki mliotuunga mkono hadi mwisho."

Kane ambaye alitolewa katika mchezo wa fainali na nafasi yake ikachukuliwa na Ollie Watkins, hiyo ilikuwa ni fainali yake ya sita akifeli kunyanyua kombe pia akishindwa kufunga hata bao moja.

Licha ya England kukosa taji, Kane alikuwa mmoka kati ya wachezaji waliopata tuzo ya mfungaji bora kwa mabao yake matatu.

Baadhi ya wachambuzi walieleza kwamba Kane ambaye alikosa taji msimu uliopita huenda alikuwa akicheza na hofu ya kushindwa ndio maana hakufanya vizuri katika mchezo huo wa fainali lakini mwenyewe alikataa hoja hiyo.

"Michuano hii inachezwa katika mazingira tofauti kama mchezaji huwa unashughulika na mengi kwa sababu sio kitu ulichozoea, niseme tu ni jinsi mashindano yalivyoisha na mchezo ulivyokuwa, ukiniuliza mimi binafsi ningependa kucheza vizuri kwenye usiku wa leo lakini haikuwa hivyo," alisema Kane muda mchache baada ya mchezo kumalizika alipokuwa akifanya mahojiano na BBC.

Chanzo: Mwanaspoti