Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize kuongoza mapokezi ya Pamba FC Jijini Mwanza

Pamba X Harmonizeee Harmonize kuongoza mapokezi ya Pamba FC Jijini Mwanza

Mon, 29 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva, Rajab Abdul @harmonize_tz anatarajiwa kuongoza mapokezi ya Pamba FC Jijini Mwanza baada ya kikosi hicho kupanda Daraja jana baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mbuni FC ya Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda amethibitisha ujio wa msanii huyo pamoja na basi maalum litakalobeba wachezaji wa kikosi hicho.

Kikosi hicho kimerejea Ligi Kuu Bara baada ya kusubiri na kuwakata kiu mashabiki wa soka wa Jiji la Mwanza ambao wamesubiri kwa zaidi ya miaka 23, huku kocha Mbwana Makatta akiandika historia ya kuzipandisha daraja timu nne ndani ya misimu saba.

Mabingwa hao wa Ligi ya Muungano mwaka 1990 wamerejea baada ya kuitandika mabao 3-1 Mbuni FC katika mchezo wa mwisho wa Ligi ya Championship ambao umepigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo jijini Arusha.

Ushindi huo imeifanya timu hiyo kufikisha alama 67 katika nafasi ya pili ikizidiwa alama tatu na bingwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live