Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Happy birthday Leonel Messi Mfalme wa Soka

Lionel Messi Xxxxxx Happy birthday Leonel Messi Mfalme wa Soka

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa Leonel Messi (37) mchezaji na mwananchi wa Jiji la Rosario umbali wa kilomita 300 mpaka mjini mkuu wa Argentina Buenos Aires.

Messi alitoakea familia ngumu, familia ya kimasikini sana ambao walikua wakiiamini ipo siku mkombozi atapatikana bibi yake mzaa baba yake ndiye alikua akimpeleka Messi viwanjani kutazama mpira na muda mwingine akimuombea apate nafasi acheze.

Kawaida hakuna mchezaji mwenye madhara Uwanjani kama Messi kwani akishika mpira kuna mambo mawili kama ataamua kuondoka mwenyewe kupiga chenga inakulazimu umfanyie madhambi au ukabe kwa akili sana kwani ni mnyumbulifu na ni mfupi kwahiyo kumkaba inajua ngumu.

Messi ambaye anatumia zaidi guu la kushoto, akipiga chenga kuna madhara yake akienda mwenyewe kuna madhara yake akitoa pasi pia lazima ifike.

Cristiano Ronaldo na Leonel Messi historia za maisha yao zainafanana na wote ni waumini wa dini ya Roman Catholic na wote ndiyo wachezaji pendwa na maarufu Duniani kote.

Wachambuzi na wasomi wanawatukana sana lakini Messi na Ronaldo ndiyo wanasoka Matajili zaidi Duniani kuliko wengine na itakua ni vigumu kwa vizazi hivi vya Chips Pombe mademu Sifa sifa kiburi kufikia hata nusu ya mafanikio ya Messi na Ronaldo.

Ronaldo kushindwa kubeba kombe la dunia haitaondoa chochote kua yeye ni mchezaji Bora Dunia na hatari zaidi hakuna Mshamhuliaji aliewahi kutokea kama Cristiano Ronaldo hata Vijana wanaosema idol wao ni Ronaldo.

Yeye mwenyewe alishasema Wana kazi ya kufanya ili kufikia yeye maana Ronaldo anasema alianza kutumia simu akiwa na miaka 18 muda mwingi alikua akitumia kufanya mazoezi kulala mapema kwani hakua na nguzo yoyote Ile na Kwao maisha yalikua magumu.

Ronaldo aliulizwa kuhusu Messi akasema ni mchezaji Bora wa Dunia

Messi aliuzwa kuhusu Ronaldo alisema ni mchezaji Bora wa Dunia.

Ni ngumu kuwatofautisha Messi na Ronaldo na kufanya hivyo ni kuukosea mpira heshima wote ni hatari na wote wameshafanya vitu ambavyo vizazi vilivyopita na vijavyo hatudhani kama vitaweza.

Messi na Ronaldo hawatumii vilevi vyovyote. Messi ndiye muumini wa michoro ya Tattoo na hivyo ilisababishwa na yeye kua shabiki mkubwa wa David Beckham lakini amekatia bima sehemu zote alizochora tattoo.

Ronaldo hana tattoo na Hana mpango wa kuchora hauwezi kumwona kwenye kumbi za Starehe na Wala havuti Sigara wara pombe na hatumii vimiminika Soft drink kama vile Soda ili kuendelea kuuweka mwili wake sawa .

MESSI MIAKA 37 TAKWIMU ZAKE

Timu ya Taifa (Argentina)

Mechi: 183

mabao: 108

Assists: 58

Amehusika kwenye Jumla ya Magoli 166 Timu ya Taifa.

KWENYE VILABU (PSG, FC Barcelona, Inter Miami

Mechi: 872

Mabao: 729

Assists: 354

Messi akiwa na Fc Barcelona pekee yake alicheza mechi 772 alifunga Magoli 670. Kumbuka Leonel Messi amezaliwa Jiji Moja na Angle Di Maria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live