Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hapa ndipo Simba alipoteleza Kagera

Simba Kagera Droo Simba mambo magumu Kagera

Thu, 22 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba imeshindwa kuendeleza wimbi la ushindi baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Kagera Sugar ilipata bao kupitia kwa Deus Bukenya dakika ya 15 kabla ya Henock Inonga kuisawazishia Simba dakika ya 38.

Zifuatazo ni dondoo muhimu za mchezo huo;

Huu ni mchezo wa nane kwa kocha Mecky Maxime kukiongoza kikosi cha Kagera Sugar tangu alipoteuliwa Oktoba 30 akichukua nafasi ya Mkenya, Francis Baraza ambapo amefanikiwa kushinda mechi nne, sare mitatu na kupoteza mmoja.

Licha ya Simba kutoka sare katika mchezo huu ila ndio timu pekee inayoongoza kwa kufunga mabao mengi ambapo hadi sasa katika michezo 17 iliyocheza imefunga 37 huku eneo lake la ulinzi likiruhusu nyavu zake kutikiswa mara nane.

Katika jumla ya michezo 17 ambayo Kagera Sugar imecheza imetoka sare mitano, ushindi mara sita na kufungwa sita ikiwa nafasi ya sita na pointi 23.

Kwa upande wa Simba katika michezo 17 iliyocheza imeshinda 11, sare mitano na kupoteza mmoja ikisalia nafasi ya pili na pointi zake 38.

Mabao yaliyofungwa na Deus Bukenya (Kagera Sugar) na Henock Inonga (Simba) ni ya kwanza kwao msimu huu wakiwa na timu zao.

Kagera Sugar imeshindwa kuendeleza rekodi yake ya msimu uliopita wakati ilipocheza kwenye Uwanja wa Kaitaba dhidi ya Simba kwani iliibuka na ushindi wa bao 1-0 Januari 26 mwaka huu lililofungwa na nyota wake, Hamis Kiiza 'Diego'.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live